Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu
Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu
Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu
Ebook259 pages2 hours

Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mara nyingi, Wakristo wengi hawaitambui sauti ya Mungu au hudanganyika kufikiri kwamba sauti nyingine ni sauti ya Mungu. Mchungaji Tucker atawatia moyo wasomaji kwamba kwa kweli wanaweza kuisikia sauti ya Mungu kibinafsi. Atayajibu maswali haya:

  • Jinsi gani tunaweza kuijua sauti ya Mungu?
  • Jinsi gani tunaweza kuitofautisha sauti ya Mungu na sauti nyingine nyingi duniani?
  • Jinsi gani tunaweza kuepukana na udanganyifu?
  • Kuna uhusiano gani kati ya kuisikia sauti Yake na imani, haki na hekima?
LanguageKiswahili
Release dateApr 28, 2021
ISBN9781596658981
Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu

Related to Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu

Related ebooks

Reviews for Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu - Rev. Robert A. Tucker

    Sauti Ya Mungu

    Yenye Nguvu

    Kumsikia & Kumwitikia

    Robert A. Tucker

    "Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu: Kumsikia & Kumwitikia"

    Toleo 1.0 kwa Kiswahili

    Kazi hii ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu:

    "God’s Powerful Voice – Hearing & Responding to Him"

    Toleo 1.0 kwa Kiingereza

    Kimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Asubisye Mejala

    © 2003 na Robert A. Tucker

    Ubunifu wa Jalada la Mbele:

    Picha ya Jalada la Mbele imeandaliwa na Wesley Dotzert

    © 2014 na Zion Fellowship, Inc.

    Haki Zote Zimehifadhi Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoweza kutolewa tena kwa njia yoyote au kwa njia yoyote ya kielektroniki au njia ya kiufundi bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupi katika nakala au hakiki.

    Nukuu zote za Maandiko zilizotumika katika kitabu hiki zinatoka katika toleo la Biblia ya Kiswahili la Union Version isipokuwa itakapotajwa tofauti.

    Iliyochapishwa kama e-kitabu mnamo Aprili 2021

    huko Merika

    Kitabu cha E-ISBN 1-59665-898-3

    Kwa habari zaidi juu ya e-vitabu, tafadhali wasiliana na:

    Wachapishaji wa Kikristo wa Sayuni

    Ushirika wa Sayuni Ushirika ®

    P.O. Sanduku 70

    Waverly, New York 14892

    Simu: (607) 565 2801

    Usitoe malipo: 1-877-768-7466

    Faksi: 607-565-3329

    www.zcpublishers.com

    Kwa maswali juu ya vitabu vilivyochapishwa, tafadhali wasiliana na:

    Kimechapishwa Tanzania

    ISBN 1-59665-880-0

    Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na:

    Zion Fellowship Incorporated

    S.L.P 2148

    Mbeya, Tanzania

    Simu: +255 (0) 686-170157

    Barua Pepe: blviola@gmail.com

    SHUKRANI

    Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wafuatao ambao wamefanya kazi ya toleo la Kiingereza la kitabu hiki: Anne McDougall, and Leslie Sigsby

    Na kwa watu waliofanya kazi ya toleo la Kiswahili: Stan Da, Justin Kropf, Lois Kropf, Joshua Silomba, Jerome Tonde, Benjamin Viola na Richard Yalonde.

    UTANGULIZI

    "Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.

    Sauti ya BWANA ina nguvu; Sauti ya BWANA ina adhama." Zaburi 29:3-4.

    Mungu anaelewa udhaifu wa mwanadamu na kushindwa kwake kufuata amri za Mungu kwa nguvu zake mwenyewe. Katika maandiko yote, Mungu anazungumzia umuhimu wa mwanadamu kuisikia sauti Yake. Sauti Yake huwatia nguvu wale wanaosikia kile anachozungumza, ikiwawezesha kutimiza alichoagiza. Wengi, kama ilivyokuwa kwa Israeli ya zamani, hupendelea kuishi kwa kufuata sheria wanayopewa na mtu anayeisikia sauti ya Mungu. Hata hivyo, nguvu ya kufanya kile anachokiagiza Mungu huja kwa kusikia sauti Yake kibinafsi.

    "Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni" Yohana 10:4-5.

    Wengi wanazifuata sauti za wageni siku hizi. Hebu tuiweke mioyo yetu katika hali ya kuisikia na kuitambua sauti ya Mungu na kumwitikia kikamilifu.

    "Wewe ukaaye bustanini, Hao rafiki huisikiliza sauti yako; Unisikizishe mimi." Wimbo ulio Bora 8:13.

    SURA YA 1

    Hebu Niisikie Sauti Yako

    Je, Ni Muhimu?

    Utangulizi

    Mwaka 1980 nilifanya safari yangu ya kwanza nje ya nchi (ng’ambo) kwenda Visiwa vya Ufilipino. Kwa sababu sikuwa msafiri mzoefu, nilijisajili kwa ajili ya safari ya ndege ya kwenda lakini si ya kurudi. Baada ya kuwasili Manila, nilijaribu kupata usajili wa safari ya kurudi ili nisafiri wiki mbili baadaye. Shirika la ndege liliniambia kuwa hawakuwa na nafasi. Waliongeza jina langu kwenye orodha ya kusubiri, huku wakiniacha nisiwe na uhakika na tarehe ya kurudi kwangu. Nikiwa nimesikitikitishwa kiasi na hali hiyo, nilimpigia simu mke wangu, Angeline, kumwelezea hali hiyo. Nilimwomba aombe ili niweze kupata nafasi katika ndege ya kurudi ingawa nilikuwa katika orodha ya kusubiri.

    Wiki mbili baadaye nilipokuwa nikisubiri, Angeline alipata wasiwasi juu ya kurudi kwangu nyumbani na hakupata utulivu usiku. Kabla ya saa 12 asubuhi alikuwa akisali, akimwomba Bwana faraja, huku akimwuliza ikiwa ningeweza kurudi nyumbani siku hiyo au la. Roho Mtakatifu alimgusa kusoma Biblia yake. Wakati huo hakujisikia kufanya hivyo, lakini alielewa kwamba Mungu anajua zaidi. Kujifunza kwake Biblia siku hiyo kulianza na Isaya 6. Alipokuwa akiisoma, maneno haya yalimgusa kipekee: "na kwa mawili aliruka" (mstari wa 2). Baada ya hapo alipata amani ya Mungu na ujasiri kwamba nilikuwa njiani kurudi nyumbani.

    Kabla ya saa 12 jioni (ambayo ilikuwa 12 asubuhi nyumbani Marekani) nilipanda ndege ya shirika la Manila, lakini wasafiri wenzangu hawakuwa tayari wamepanda. Walipitia kwanza Hong Kong. Walifika mara moja muda mfupi kabla ya ndege kuondoka na "na kwa mawili aliruka" kama Mungu alivyosema na mke wangu. Mungu alimpa mke wangu Neno kwa wakati mahususi kumfariji! Mungu anapenda kuwasiliana na watu wake.

    Shauku ya Mungu ya Ushirika

    Mungu alituumba kwa kupenda kwake, ili tuwe na uhusiano wa karibu na ushirika pamoja Naye. Ni jambo zuri la ajabu kwamba Mungu anataka kuzungumza moja kwa moja nasi na kutufanya tuijue sauti Yake! Maandiko yameanza na kuelezea Mungu kukutana kila siku na Adamu na Hawa katika bustani. "Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga" (Mwanzo 3:8). Inaonekana kwamba Mungu alikuja kwa mara kwa mara kukaa pamoja nao katika ushirika.

    Kitabu cha mwisho cha Biblia kinaonyesha moyo na shauku ya Mungu kuwasiliana na mwanadamu na kutufanya tuisikie sauti Yake. "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami" (Ufunuo 3:20). Huu ni mwaliko mkuu sana hasa ukizingatia kwamba Mungu ndiye muumbaji na mtawala wa ulimwengu! Kwa kulizingatia hili, Mfalme Daudi alinena, "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke?" (Zaburi 8:4). Mungu anawatafuta duniani kote wale watakaoitikia sauti Yake na wenye shauku ya ushirika na Yeye. Kama tutakavyoona katika somo hili, maandiko yana mialiko kadhaa vya kuisikia sauti ya Mungu.

    Kwa nini ni muhimu sana kuisikia sauti ya Mungu? Je, kuna umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Yeye? Mtu anawezaje kuujua utofauti wa sauti ya Mungu na sauti nyingine zote duniani? Mtu anawezaje kuhakikisha kwamba ni kweli Mungu ndiye anayesema? Ni kwa vipi mada kama vile imani, tumaini, matendo mema, haki, na hekima zinahusiana na kuisikia sauti ya Mungu? Hili ni somo la kusisimua ambalo litatoa majibu ya maswali haya na mengine ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu mada hii. Weka moyo wako wazi kwa Bwana tunapopitia kitabu hiki na uone kama unaisikia sauti Yake ikikuita. Sema pamoja na mwandishi wa Wimbo ulio Bora, Hao rafiki huisikiliza sauti yako; Unisikizishe mimi (8:13).

    SURA YA 2

    Jambo la Muhimu

    Mfano wa Israeli

    Akiliandikia waraka kanisa la Korintho, Paulo anawaonya kutafakari mfano wa Israeli katika safari ya jangwani kutoka Misri kwenda Kanaani. Anaelezea kushindwa kwao na analionya kanisa kutokufanya makosa sawa na yaliyofanywa, na Israeli.

    Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; Wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mambo mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano; yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke (1 Wakorintho 10:1-12).

    Safari ya Israeli kupitia jangwani ilitawaliwa na kushindwa kwingi. Kushindwa kwa aina fulani kulijitokeza zaidi. Inawezekana kutambua sababu kuu za kuongezeka kwa matatizo yanayojitokeza. Hili lilikuwa na ukweli kabisa kwa Israeli ya wakati ule. Hebu tuangalie sababu moja kuu iliyofanya kizazi cha kwanza (cha Israeli) kushindwa kuingia katika ahadi (nchi ya ahadi) na badala yake kufia jangwani.

    Wito Mkuu wa Mungu

    Israeli walianza safari yao kutoka Misri usiku wa Pasaka. Walivuka Bahari ya Shamu na kufika Mlima Sinai siku hamsini baadaye. Mungu aliwapeleka huko na kuwaandaa ili aweze kuzungumza nao. Haya ndio aliyowaambia awali:

    Musa akapanda kwa Mungu; Na BWANA akamwita toka mlima ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli maneno haya; Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. Sasa basi, ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote  pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli (Kutoka 19:3-6).

    Mungu aliwaambia Waisraeli kuwa atawafanya kuwa ufalme wa makuhani na taifa takatifu iwapo wangemwitikia kwa njia mbili – kutii sauti Yake na kulishika agano Lake. Hii ni ahadi kuu sana!

    Katika Kutoka 20 Mungu aliwapa agano hilo – Amri Kumi. Mungu alizungumza nao kutoka Mlima Sinai pamoja na madhihirisho makuu ya Nguvu Zake.

    Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia; basi Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi. Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu ambalo Mungu alikuwapo (Kutoka 20:18-21).

    Watu waliogopeshwa sana na yote yaliyotokea. Musa alijaribu kuwatuliza watu na kuwaelezea yaliyotokea. Mungu hakutaka kuwaogopesha. Alitaka kuwajengea hofu ya Bwana ambayo ingeweza kuwahifadhi na kuwazuia wasitende dhambi. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu (Mithali 16:6). Mungu alikuwa akiwatia moyo Waisraeli wasiogope matukio ya asili au moto Wake ulao uliokuwa ukiwaka ndani ya roho zao. Aliwataka kumcha Bwana na kumheshimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Yesu alizungumza vivyo hivyo na wanafunzi Wake. Msiwaogope wale wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanum (Mathayo 10:28).

    Kuelezewa tena kwa tukio hili katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati kunatupa picha kamili, inayojitosheleza zaidi ya tukio hili. Tunaona kwamba Israeli walikataa kusikia kutoka kwa Mungu.

    BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto, (Nami wakati ule nalisimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonyesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani) ... Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa. Ikawa, mlipoisikia ile sauti toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa kabila zenu, na wazee wenu; mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonyesha utukufu wake, na ukuu wake; nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwandamu, naye akaishi. Sasa basi mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa. Maana katika wote wenye mwili wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi asife? enenda karibu wewe, ukasikie yote atakayosema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda (Kumbukumbu la Torati 5:4-5; 22-27).

    Mungu Anapozungumza, Mwanadamu Hupata Uzima

    Mwitikio wa kwanza wa Israeli kwa Musa ulikuwa kwamba Mungu anapozungumza,  uzima huingia ndani ya mwanadamu. Ukweli huu unathibitishwa na maandiko kadhaa yanayodhihirisha uwezo wa Mungu ambao huachiliwa (hutolewa) wakati anapozungumza. Uzima hububujika maneno ya kinywa chake yanapotoka.

    Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi. Sauti ya BWANA ina nguvu; Sauti ya BWANA ina adhama; Sauti ya BWANA yaivunja mierezi; Naam, BWANA aivunja – vunja mierezi ya Lebanoni; Airusha – rusha kama ndama wa ng’ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana – nyati. Sauti ya Bwana yaipasua miali moto. Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa; BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi. Sauti ya BWANA yawazalisha ayala, na kuifichua misitu; na ndani hekalu lake Wanasema wote, Utukufu (Zaburi 29:3-9).

    Atoapo sauti yake pana mshindo wa maji mbinguni; Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Hifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake (Yeremia 51:16).

    Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wale waisikiao watakuwa hai (Yohana 5:25).

    Mungu anapozungumza, nguvu hutoka katika sauti Yake na vitu huanza kutokea! Hata wafu hufanywa kuwa hai tena katika kuzungumza kwake! Yesu pia alisema, maneno hayo niliyowaambia, ni roho, tena ni uzima (Yohana 6:63). Maafisa walipokuja na Yuda katika bustani ya Gethsemane, Yesu aliwauliza waliyekuwa wakimtafuta. Wakamjibu kwamba walikuja kumtafuta Yesu wa Nazareti. Aliposema, "NI MIMI", nguvu nyingi ziliambatana na sauti Yake (Yesu) kiasi kwamba walirudi nyuma wakaanguka chini (Yohana 18:3-6).

    Israeli walitangaza siku hiyo kwenye Mlima Sinai kwamba waliiona na kuielewa nguvu iliyokuwemo katika sauti ya Mungu na uzima uliobubujika kwenda kwa mwanadamu Mungu alipokuwa akizungumza. Oh! Kama wangeendelea kuwa waaminifu kwa kulielewa hilo! Nguvu yote waliyohitaji ili kulitunza agano ilikuwepo kwa ajili yao iwapo wangeitii sauti Yake.

    Kwa Nini Tufe?

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1