Vous êtes sur la page 1sur 9

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 1 of 9

Maskani

Makala

Burudani & Michezo Tuwasilane

Barua

Tahariri

Kura ya Maoni

Hifadhi

Pekua tovuti
Makala

Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa


Mbaraka Islam
Toleo la 282 20 Feb 2013

Maoni ya Wasomaji
Ni kweli Nyerere hakuwa MUNGU lakini sihamni kama hakuwa MTUME wake kwani hata manabii wote wa MUNGU kuna mapungufu yao ndiyo maana walikuja wengi na kwa wakati tofauti.

KWA takriban miaka mitano sasa, raia mmoja wa Uingereza, Sarah Hermitage amekuwa akiendesha kampeni ya kumchafua Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania, taasisi muhimu za nchi yetu kama vile mahakama, waandishi wa habari na hata Watanzania ambao wamekua wakimpinga.

12 hours 47 min

Pamoja na kuwa kumekua na mapungufu katika serikali yake na vyombo vyake kama ilivyo kwa serikali nyingine Duniani ikiwamo ya Uingereza, Muingereza huyu amekua akitoa kashfa kwa kila jambo linaloandikwa ama kujadiliwa kuhusiana na viongozi wa Tanzania na taasisi zake na kwa kutumia lugha isiyo na staha.

Yametolewa maoni mengine 4


ziada

Makala Pendwa
Akaunti ya kigogo

TANESCO yazuiwa
Waandishi Wetu 25,498

Meseji za komredi

Lowassa zanaswa
Mwandishi Wetu 23,559

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 2 of 9

Watanzania siku zote wakiwamo wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati, wamekua wakiikosoa na hata kuishambulia serikali na vyombo vyake inapokosea jambo ambalo ni jema na linasaidia kuimarisha utawala bora, lakini kwa staili anayotumia Muingereza huyu ni kupitiliza mipaka na zaidi ya yote ni udhalilishaji usioweza kuvumilika kwa mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake. Dhumuni la Sarah Hermitage na washirika wake wakiwemo baadhi ya Watanzania ni kuzishawishi nchi za Magharibi wakianzia na Uingereza kusitisha misaada na uwekezaji katika Tanzania. Hilo angeweza kulifanya huko kwao kwa kuwasiliana na serikali yake, lakini badala yake amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na barua pepe tena kwa kutumia lugha ya kukashifu na kudhalilisha.

Spika, Waziri Mkuu

wamuonya Kikwete
Mwandishi Wetu 21,671

Mambo hadharani
Waandishi Wetu 20,253

Wamo vigogo

wawili wastaafu
Mwandishi Wetu 19,563
ziada

Kura ya Maoni
Gesi ya Mtwara ibaki Mtwara? Ndiyo

Watanzania wote tuna jukumu la kutetea heshima ya nchi yetu, lakini wapo wale ambao tumewapa jukumu la kusimama mstari wa mbele. Jambo la kusikitisha ni kwamba ni watu wachache sana kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ambaye amekua na ujasiri wa kumkabili Muingereza huyu, kwa kumwambia wazi kwamba kama ni misaada ana haki ya kuishawishi nchi yake kuzuia misaada kwa Tanzania lakini si kwa kudhalilisha Watanzania. Zitto alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba nchi nyingi tajiri duniani ikiwamo Uingereza, zimejengwa kwa kutumia rasilimali walizozipora katika nchi walizozitawala ikiwamo Tanzania na kwamba nchi hizo zinaweza pia kuendesha shughuli zake bila misaada ya dharau.

Hapana
Piga kura
Yaliyopita Matokeo

Tunapatikana Facebook
Raia Mwema
Like 968 people like Raia Mwema

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 3 of 9

Bahati mbaya sana watendaji wengine wengi ambao wanapaswa kutetea heshima yetu, hili suala limewapita, pengine kutokana na kutokua na taarifa sahihi ama kwa kutowajibika. Jambo la kujiuliza, wale ambao miongoni mwa majukumu yao ya kila siku ni kutetea na kulinda hadhi na heshima ya nchi yetu wanafanya kazi gani? Sasa tunawalipa mishahara mikubwa na marupurupu ya nini kama hawawezi kututetea tunapodhalilishwa ama kutukanwa?

Mada Moto
RichmondWarioba

Katiba

MpyaMuungano
50PindaMkapa

Bunge

NyerereBoTMbeya
Lango la Wenyeji
Jina * Siri *

Hali hii inatufanya tukumbuke ujasiri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara kadhaa aliwatunishia misuli viongozi wa mataifa makubwa walipotaka kuidhalilisha nchi yetu, sembuse raia mmoja ambaye amekua akitumia matatizo yake binafsi kutaka kuidhalilisha Tanzania na kutaka kuishinikiza serikali yake na nyingine kuichukia Tanzania. Jinsi anavyotumia mtandao wa twitter kuchafua Tanzania Sarah Hermitage amekua akitafuta katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania vinavyoandika taarifa zozote kuhusu Tanzania na kuziongezea maneno ya kukashifu na kejeli. Kwa mfano amekua amechukua taarifa inayomunukuu Raia Jakaya Kikwete akiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupambana na rushwa hadi ndani ya Baraza la Mawaaziri, na yeye kuongezea maneno akisema, kundi moja la majambazi linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi.
Jisajili Badilisha siri
Tuma

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 4 of 9

Akachukua taarifa iliyochapishwa katika vyombo vya habari ikimnukuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribisha wawekezaji katika kilimo na yeye kuongeza maneno akisema, Mheshimiwa Pinda kitakachoendelea kukandamizi uwekezaji katika kilimo cha Tanzania ni uporaji wa ardhi ya wawekezaji katika mtindo wa Mugabe (Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe). Amekua akidiriki kukashifu hadi majaji wote wa Tanzania kwamba wana bei akisema, sina hakika kama unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei, kauli ambayo hata Watanzania wanakua wakiitoa kwa uangalifu maana hata kama kuna majaji ambao si waadilifu, haiwezekani wakawa ni wote, kama ilivyo katika taasisi nyingine. Raia mmoja wa Kenya anayeishi Tanzania, aliyejitambulisha kwa jina la Marigi Patrick aliandika katika mtandao kwa kusema; Sisi Wakenya tuna matatizo yetu na tumekua na tofauti kubwa sana za wazi wazi, lakini anapotokea raia wa kigeni kumshambulia kiongozi wetu tena kama Rais wa nchi, tunaungana na kumshughulikia. Kuna wakati Wazungu walimshambulia Rais Mwai Kibaki, sote tukisaidiwa na wabunge wetu na vyombo vya habari tulimshambulia hadi akakoma kutudharau. Marigi ambaye anajihusisha na biashara ya bima, anasema Watanzania bado ni wachanga katika demokrasia, ama wanadharau kila kitu bila kujua madhara yake katika hadhi na heshima ya Taifa, na

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 5 of 9

ndio maana wanashindwa kutofautisha kati ya demokrasia na udhalilishaji unaofanywa na raia wa nchi nyingine kama alivyo Sarah Hermitage. Soma zaidi kuhusu:
Sarah Hermitage

Tufuatilie mtandaoni:
Like 3

Wasiliana na mwandishi

Mbaraka Islam

Endelea Kuhabarika
Changamoto za vyombo vya habari katika demokrasia ya Tanzania Changamoto za vyombo vya habari katika demokrasia ya Tanzania II Tanzania yetu: Kutoka misingi ya utu hadi katika uvutaji bangi Dhima ya vyombo vya habari katika demokrasia ya vyama vingi

Maoni ya Wasomaji
Viongozi dhaifu wataona wapi
Permalink Submitted by Achebe Nyandeka (not verified) on Mon, 2013-02-25 16:28.

Viongozi dhaifu wataona wapi mambo kama haya wakati hawana utamaduni wa kusoma. Na hata kama raia mwema imewafunulia waulize mpaka sasa wamechukua hatua gani kwa Nyang'au kama huyu.
reply

Huyu mama ni mkosaji tu.

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 6 of 9

Permalink Submitted by Kichuguu (not verified) on Mon, 2013-02-25 19:14.

Huyu mama ni mkosaji tu. Aligombana na Benjamin Mengi kuhusiana na ununizi wa shamba la overdale kwa dola 130,000 ambazo alishindwa kulipa in time. Kuanzia hapo akamdandia Reginald Mengi akitaka apate kitu kwa vile anajua kuwa Reginald ni tajiri, akasindwa; alipojua kuwa kuna rift kati ya Mengi na Yusuf Manji akaamua kumdandia Manji kujenga urafiki ili amtumie Manji kumkamua Mengi, bado akagonga mwamba, akapiga kelele kwenye kampuni ya Kokakola huko Atlanta kusudi imnyanganye mengi ile franchise ya Bonite Bottlers akagonga mwamba, akapeleka barua World Bank kuitaka isitishe ule msaada iliokuwa imetoa kwa makampuni ya Mengi akagonga mwamba. Ni mama maskini aliyekuwa anataka kuneemekea Tanzania akaula wa chuya.
reply

Wenzetu wakiudhiwa na
Permalink Submitted by Jaribu (not verified) on Mon, 2013-02-25 21:35.

Wenzetu wakiudhiwa na serikali zao hupiga makelele mpaka wapate tamati. Sisi tukionewa, kuibiwa na kunyanyaswa na viongozi wetu tunaomba dua tu wadhurike siku ya kiyama. Stori ya huyu mama na mmewe inasikitisha, kwa sababu ni mambo yanayotokea wananchi wa kawaida Tanzania kila siku; tofauti ni kwamba yeye hanyamazi na kuomba dua. Angekuwa ni mzungu tapeli mwenye hela za kutosha kuhonga yasingemfika yanaliyomfika. Labda atawahamasisha Watanzania wachangamke na kuwatimua vilaza wezi wanaotuongoza. Hata makaburu wa Afrika Kusini nao walitumiliwa baada ya mataifa makubwa kuwawekea vikwazo vya uchumi. Hata nao waliona kuwa wanatukanwa bila sababu!

reply

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 7 of 9

Wewe Mbaraka Islam ni


Permalink Submitted by Mzee Pembe (not verified) on Thu, 2013-02-28 17:53.

Wewe Mbaraka Islam ni kibaraka mkubwa kabisa. Unataka tutetee uozo wakati yote anayosema huyu mama ni kweli tupu. Ni kipi alichodanganya hapo. Unataka awe mnafiki na mwoga kama sisi Watanzania tunavyokaa kimya wakati haya majambazi yanatuibia. Nimemwandikia huyu mama email na kumwezeza jinsi unavyotaka kutulisha mawazo potofu yaliyozoza. Sikujua wewe ni mtu wa hovyo namna hii!
reply

Nakuunga mkono ndugu Islam


Permalink Submitted by George Mwita (not verified) on Thu, 2013-02-28 20:05.

Nakuunga mkono ndugu Islam kwa kulileta hili. Tumekosa uzalendo wa kulitetea taifa letu na viongozi wetu ndani na nje ya nchi. Waandishi wa Kitanzania wakisikia hoja imetolewa dhidi ya nchi yetu huirukia na kuiunga mkono. Hiyo si sahihi hata ikiwemo ukweli wowote yapo maelezo ya kizalendo tunaweza kuyatoa kujibu hoja potofu za wasiotupenda na hapo tunapata heshima tuliiponda nchi yetu hatutapati sifa bali tunadharaulika tu. kwa Mfano mie sikubali kama Tanzania inaongoza kwa ushirikina duniani na nilitoa mawazo yangu gazetini.
reply

<p>Huyu mama anaweza kujua


Permalink Submitted by Msomaji wetu (not verified) on Mon, 2013-03-04 14:08.

Huyu mama anaweza kujua matatizo yetu kulikoni sisi wenyewe ?? kwani yeye ni nani?? aanze kwanza kutatua matatizo ya nyumbani kwake na mumewe then na nchi yake .... Ndipo Haanagalie watu wengine!! kwa mtazamo wangu ana lake jambo na Tanzania

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 8 of 9

yetu..sababu ukiangalia nchi za ki-africa zote zina matatizo ila yanazidiana lkn sisi tuna nafuu kati ya hizo...mwambie atambae zake....
reply

Wasome zaidi Waandishi wa Raia Mwema

Toa maoni yako


Your name

E-mail
The content of this field is kept private and will not be shown publicly.

Homepage

Comment *

Switch to plain text editor


More information about text formats Text format Filtered HTML
Web page addresses and e-mail addresses turn into links automatically. Allowed HTML tags: <a> <em> <strong> <cite> <blockquote> <code> <ul> <ol> <li> <dl> <dt> <dd>

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Raia Mwema - Tanzania yatukanwa na Muingereza, huku wakubwa wakizubaa

Page 9 of 9

Lines and paragraphs break automatically.

What code is in the image? *


Enter the characters shown in the image.

Save

Preview

Lula wa Ndali Mwananzela Johnson Mbwambo Joseph Mihangwa John Bwire Maggid Mjengwa Privatus Karugendo Hidaya Jenerali Ulimwengu Godfrey Dilunga Ayub Rioba

Ahmed Rajab Evarist Chahali Paul Sarwatt Chesi Mpilipili Felix Mwakyembe Ibrahim Mkamba Msomaji Raia Deus Bugaywa Mayage S. Mayage Francis Chirwa

Innocent Mwesiga Aristariko Konga Deusdedit Jovin Ncheme Nchicheme? Paul Dotto Zitto Kabwe John Daniel Kitila Mkumbo Ezekiel Kamwaga Mary Victor

Julius Sarota Andrew Bomani Damian M. Gabagambi Bullet Straton Ruhinda Marie Shaba Yahya Msangi Njelu Kasaka Selemani Rehani Mkami Msami Baptiste Mapunda

Copyright 2013 Raia Mwema Newspaper Company unless otherwise noted. All rights reserved.

http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-yatukanwa-na-muingereza-huku-wakubwa-wakizu... 11/03/2013

Vous aimerez peut-être aussi