Vous êtes sur la page 1sur 28

SHERIA YA KULINDA ARDHI YA KILIMO

MADA KATIKA WARSHA YA WA WADAU WA KILIMO, BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO PLAZA, TAREHE 2 DESEMBA, 2013 GEORGE MANDEPO
Afisa Sheria Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

UTANGULIZI
Ardhi ni rasilimali kuu ya kwanza, Kilimo kinafanyika juu
ya ardhi, Rasilimali nyingine muhimu ni maji, pembejeo na nguvu kazi. Sera mpya ya Kilimo (2013):
- Tanzania in kiasi cha takriban Hekta 44 milioni za ardhi (arable

land ) - hekta 10.8 milioni sawa na 24% ndio zinazolimwa mazao kwa sasa (under crop production). - Mfumo wa sasa wa umiliki ardhi (;land tenure) hauwezeshis kuleta mabadiliko ya haraka nwenye kilimo. - Kulindwa kwa ardhi inayofaa kwa kilimo ni muhimu kwa uwekezaji endelevu

- Ardhi kwa ajili ya kilimo ni mojawapo ya nguzo za KILIMO

KWANZA (Nguzo Na.5 Ardhi kwa Ajili ya Kilimo KwanzaWizara ya Ardhi na Serikali za Mitaa kutambua, kutenga na kutangaza katika gazeti la Serikali ardhi kwa ajili ya uzalishaji mazao na ufugaji).

UTANGULIZI.
Kwa kuzingatia mazingira ya kisheria ya sasa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo (large-scale farming investment) sio rahisi sana; wakulima wadogo wanaogopeshwa na ujio wa wakulima wakubwa/wawekezaji. Msuguano wa kugombea ardhi kati ya sekta ya

Kilimo na sekta zingine (mifugo, madini na mali asili kama misitu na wanyama pori. Sera na sheria zilizopo zinahitaji kuhakikisha kuwa kilimo kinaendelea kuwa sekta kiongozi katika uchumi wa nchi.

SHERIA NA SERA MBALIMBALI


Kutungwa kwa Sera ya Ardhi 1995, ambayo ilifuatiwa na

Sheria za Ardhi mwaka 1999; Kwa mujibu wa Sheria za Ardhi za Tanzania (Sheria ya Ardhi, Na. 4 (1999) na Sheria ya Ardhi ya Vijiji, No. 5, 1999) ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na inamilikiwa na Rais kwa niaba ya umma wote wa watanzania; Sheria ya Ardhi inagawanya ardhi katika makundi makuu mawili: (a) ardhi ya jumla (general land) na (b) ardhi iliyotengwa kwa mujibu wa sheria (reserved land) Ardhi ya jumla ni ile ambayo haijatengwa kwa mujibu wa sheria, ikiwemo Sheria ya Ardhi ya Vijiji (No. 5/ 1999) Kwa kuwa ardhi ya kilimo haijatengwa hivyo ni sehemu ya ardhi ya jumla;

MGAWANYO WA ARDHI KATIKA SHERIA ZA ARDHI


Sheria za ardhi na Ardhi ya Kijiji zinaweka utaratibu wa

jinsi ya kupata, kutumia, kusimamia na kumiliki ardhi. Sheria ya Ardhi Na. 4/1999 inasimamiwa na Waziri mwenye dhamana ya ardhi kupitia kwa Kamishna wa Ardhi ili kuhakikisha kuwa malengo ya kutungwa kwa Sheria hii yanatekelezwa Kikamilifu. Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5/1999 inasimamiwa na Mabaraza ya Vijiji (Village Councils) kwa kuangalia ardhi hiyo kwa niaba ya Mikutano ya Vijiji (Village Assemblies) ambayo yapo kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa ( (The Local Government (District Authorities Act) Sura ya 287.

MGAWANYO WA ARDHI KATIKA SHERIA ZA ARDHI


Sheria ya Ardhi Na.4 imeigawa ardhi katika makundi matatu(3) (Kifungu cha 4(4)):

Ardhi ya Jumla (general land) : ardhi ambayo siyo ya hifadhi na ardhi ya kijiji ambayo haikaliwi wala haitumiki (inasimamiwa na Kamishna wa Ardhi). Ardhi ya Vijiji (village land ): Ardhi ndani ya mipaka ya vijiji chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya 1982 na Sheria ya Makazi ya 1965; Ardhi inayomilikiwa na wanakijiji kwa muda usiopungua miaka 12 kabla ya tarehe 1 Mei 2001 (inasimamiwa na Halmashauri ya Kijiji).

MGAWANYO WA ARDHI KATIKA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI ,1999


Sheria ya Ardhi ya Kijiji inaelekeza Mabaraza ya Vijiji

kugawa ardhi yao katika makundi tatu: (i) Ardhi ya Jumuiya : inayotumiwa na watu wengi kijijini inayojumuisha misitu, maeneo ya malisho au maeneo mengine yenye maliasili yanayosimamiwa na vikundi vya watu isigawiwe kwa mtu yeyote binafsi itakayojulikana kama ardhi za kijiji za jumuiya (ii) Ardhi inayokaliwa: imegawiwa na inatumiwa kwa ujenzi wa nyumba, kilimo, biashara n.k. na watu binafsi au familia mojamoja. (iii) Ardhi ya matumizi ya baadaye: Inatengwa kwa matumizi ya baadaye ya watu binafsi au jumuiya.

MGAWANYO WA ARDHI KATIKA SHERIA ZA ARDHI..


- Ardhi ya Hifadhi (reserved land ) : Ardhi iliyotengwa kwa madhumuni maalum . - Imetambuliwa kisheria chini ya Kifungu cha 6 cha Sheria za Ardhi. - Inasimamiwa na Sheria maalumu (Sheria ya Misitu; sheria ya Hifadhi ya Mbuga za Wanyama, Sheria ya

Hifadhi ya eneo la Ngorongoro; Ardhi yenye majimaji (kama ile iliyo pembezoni mwa mito na madimbwi); Hifadhi ya barabara; Maeneo ya wazi (kama yale yaliyotengwa kwa ajili ya kupumzikia, burudani, michezo na starehe)
la Hifadhi.

- Mhe. Rais au Waziri husika ana mamlaka ya kluitangaza . - Baadhi ya Sheria za Hifadhi zinazuia hata kuingia katika eneo

SHERIA ZA ARDHI YA HIFADHI


Sheria ya Hifadhi za Taifa sura ya 282 (National Parks Act) inampa mamlaka Mhe. Rais kutangaza eneo lolote kuwa hifadhi ya Taifa (kf.3) Sheria ya Hifadhi ya Bahari (Marine Parks and Reserves Act) sura ya 146 Waziri mwenye mamlaka anaweza kutangaza ardhi hifadhi ya bahari. Kifungu cha 42 cha kinazuia shughuli nyingine zozote za kiuchumi (commercial activities) kwenye eneo lililotangazwa kuwa hifadhi. Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori (The Wildlife Conservation Act) sura ya 283. Kifungu cha 15 kinazuia

mtu yeyote kuingia eneo la hifadhi isipokuwa kama anasafiri au ana kibali ya Mkurugenzi wa Wanyamapori.

SHERIA ZA ARDHI NA ARDHI YA KILIMO


Sheria za Ardhi zinatambua Ardhi ya Hifadhi (reserved

land ) ambazo ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Lengo mahususi la kuwa na ardhi ya hifadhi ni kuhakikisha kuwa ardhi hizo zina lindwa, kuendelezwa na kuzifanya zisitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Miongoni wa ardhi zinazotajwa chini ya ardhi za hifadhi kwenye sheria za sasa za Ardhi, ardhi kwa ajili ya kilimo haipo japokuwa kwa nadharia inaonekana kuwa nchi ina ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo

MAPUNGUFU KATIKA SHERIA ZA ARDHI KUHUSU MAENDELEO YA KILIMO


Sheria zilizopo za Ardhi, zimejikita kwenye kusimamia

upatikanaji na umiliki wa ardhi na kulinda haki za wamiliki wa ardhi. Hazijabainisha kwa kina utaratibu mzima wa kusimamia uendelezaji wa ardhi kwa kuzingatia madhumuni ya kumilikishwa kwake Masharti ya kumtaka mmiliki wa ardhi kuzingatia kanuni zilizo chini ya Sheria nyingine kwa mfano, kuzingatia mbinu za kilimo bora, kuhifadhi mazingira, kutumia maliasili nyingine kama vile maji nk kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika kitaalamu nk. Hayahusihwe na masharti ya hatimiliki.

MAPUNGUFU KATIKA SHERIA ZA ARDHI KUHUSU MAENDELEO YA KILIMO Mamlaka za usimamizi wa ardhi zinaweza kubatilisha hatimiliki ikiwa mmiliki atashindwa kuzingatia masharti yanayoambatana na haki ya kumilikisha (hatimilki). Kwa mtu ambae anamiliki au kuikalia ardhi kwa jinsi yeyote ile pasipokuwa na hatimiliki akishindwa kuendeleza ardhi husika, anaweza kutochukuliwa hatua zozote kwani kisheria hatambuliki . Hii inaweza kudhohofisha mipango mingine ya maendeleo, kwani Serikali inapopeleka huduma za kilimo kwa wakulima ikiwemo ruzuku za pembejeo, zana na huduma za ugani, haiangalii iwapo Mkulima husika ana haki yeyote ya kisheria ya kuitumia ardhi ambayo uzalishaji unaendelea.

MAPUNGUFU KATIKA SHERIA ZA ARDHI KUHUSU MAENDELEO YA KILIMO


Wakati wa Ukoloni, kulitungwa Kanuni za Ardhi (Land

Regulations, 1948) ambazo ziliwataka wamiliki wa ardhi kwa ajili ya kilimo kuendeleza ardhi kwa viwango fulani vinginevyo wangenyanganywa ardhi hiyo. Ardhi ya kilimo inapaswa kutumika kwa kupanda mazao, mifugo nk, Sheria ilipaswa kuhusisha mamlaka zinazosimamia kilimo kutambua viwango vya uendelezaji wa ardhi katika kufikia maamuzi ya kuchukua hatua dhidi ya mmiliki wa ardhi husika. Halmashauri za Wilaya, zimekuwa ikitunga Sheria ndogo (By- Laws) za kuendeleza kilimo kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mtaaa, Sheria hizo ndogo haziwezi kutekelezwa kwa ukamilifu kutokana na kukosa msukumo wa kitaifa.

AZMA YA KUITAMBUA NA KUILINDA ARDHI YA KILIMO


Sera mbalimbali za nchi zinatambua umuhimu wa kuainisha, kupima na kulinda ardhi ya kilimo ili

itambulike na kutumika kwa madhumuni ya kilimo na sio vinginevyo. Sera hizo zina weka misingi ya kuwa na mfumo wa kisheria wa Sheria wa kulinda rasilimali hiyo muhimu kama ilivyo kwa rasilimali nyingine kwa mfano maji. Mwaka 2002, Serikali ilipitisha Sera ya Maji ya mwaka 2002 (The National Water Policy, 2002) na mwaka 2009 ilitunga Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali Maji (The Water Resources Management Act 2009). Lengo kuu la Sera na Sheria ya Maji ni kuweka mfumo mzuri wa kupata na kutumia rasilimali maji na kulinda vyanzo vya maji

MFUMO WA SHERIA YA ARDHI YA KILIMO


Maandalizi ya Mfumo wa Sheria ya Kulinda Ardhi ya

Kilimo yalianza toka mwaka, 2007 ambapo kupitia mapendekezo ya rasimu ya Mpango Kabambe wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo (National Agricultural Land Use Master Plan) ilionekana kuwa ipo haja ya kuwa na sheria itakayotambua, kuainisha, kulinda na kuendeleza ardhi ya kilimo ili iweze kutumika kwa kuzingatia umuhimu wake. Kama ilivyo kwa sekta nyingine zinazotegemea ardhi, kilimo kikiwa ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi, kinahitaji kuwa na ardhi inayotambulika kitaalamu na itakayolindwa ili isiweze kuvamiwa na shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo makazi nk.

MFUMO WA SHERIA YA ARDHI YA KILIMO..


Utekelezaji wa marekebisho katika sera na sheria za ardhi umeleta migogoro ya ardhi ambayo inasababishwa

na:
Kutokuwepo kwa Mpango Kababe wa Matumizi bora ya ardhi

unaozingatia haki za wahusika mbalimbali katika ardhi; Kuendelea kuhama hama kwa watu mbalimbali kutafuta ardhi kwa ajili ya malisho, kilimo na makazi; Kugombania vyanzo vya maji; Kuendelea kuwepo kwa ardhi ambayo haijapimwa na kugawiwa kwa vijiji au wawekezaji; Uwekezaji usiozingatia haki za wenyeji; Kutokuwepo mfumo madhubuti wa utatuaji wa migogoro ya ardhi, hususan katika ngazi za vijiji.

CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA MAPUNGUFU KATIKA SERA NA SHERIA


Mapungufu katika Sera na Sheria za Ardhi zinajitokeza changamoto zifuatazo: Kuendelea kuwa na kilimo ambacho hakikidhi malengo ya Taifa kutokana na kutokuwa sheria inayolida na kusimamia kilimo cha Tanzania; Wawekezaji katika ardhi ya kilimo kuendelea kutumia ardhi hiyo kwa malengo ambayo hayakukusudiwa wakati wa kuanza uwekezaji; Ardhi kwa ajili ya wakulima wadogo kuendelea kuhawilishwa kwa wakulima wakubwa au wawekezaji bila utaratibu maalum; Wafungaji kuvamia na kuchukua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha mazao na misitu; Ufugaji usiosimamiwa au kuthibitiwa; Uongezwaji wa maeneo yanayolindwa na sheria kama vile ya wanyama pori, misitu na ardhi oevu; Uharibifu wa mazingira kwa ujumla unaosababisha mabadiliko ya tabia nchi n.k

SERA NA SHERIA ZINAZOTAMBUA UMUHIMU WA ARDHI YA KILIMO..


Mbali na Sera na Mikakati iliyokwisha twaja awali kuhusu maendeleo ya kilimo ikiwemo ASDS, Nguzo ya 5 ya KILIMO KWANZA inafafanua kwa kina nia ya kuwa na Ardhi ya kilimo kwa kutambua umuhimu wake. Katika nguzo hii, imebaishwa wazi kuwa ni jukum la Wizara ya Ardhi na Serikali za Mitaa kutambua, kutenga na kutangaza katika gazeti la Serikali ardhi kwa ajili ya uzalishaji mazao na ufugaji. Nguzo hii pia inataka uandaaji wa mipango miji uzingatie pia utengaji wa ardhi ya ukanda wa Kilimo (Agricultural Green Belts); Mikoa kuanzishwa Benki za Ardhi (land Bank) kwa ajili ya uwekezaji wa kibiashara katika kilimo na kupitiwa upya kwa Sheria ya Uwekezaji ili kuwezesha wazawa kuingia ubia na wawekwezaji wanaomiliki ardhi kupitia TIC .

SERA NA SHERIA ZINAZOTAMBUA UMUHIMU WA ARDHI YA KILIMO..


Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (The Land Use

Planning Act No. 10/2007) inabainisha katika Kifungu cha 28 (1) (a) na (k) kuwa, katika kuandaa mipango ya ardhi, mamlaka husika zinapaswa kujuisha mapendekezo ya kutambua ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao, nyanda za malisho (rangeland), misitu, vyanzo vya maji, uvuvi, ukulima, viwanda nk. Vifungu vya 3 na 7 vya Jedwali la pili (Second Schedule) na Kifungu cha 2 cha Jedwali la Tano (Fifth Schedule) vinabainisha nia ya kuitambua ardhi ya kilimo katika maandalizi ya mipango ya ardhi ya Mikoa, Wilaya na Vijiji

SHERIA ZINAZOTAMBUA UMUHIMU WA ARDHI YA KILIMO..


Sheria ya Nyanda za Malisho na vyakula vya Mifugo (the Grazing-land and Animal Feed Resources Act, 2010)

kwa ajii ya kusimamia ardhi ya nyanda za malisho. Sehemu ya Sheria hii inayohusu nyanda za malisho. Imerejesha sheria ya Maendeleo ya Nyanda za Malisho (Range Development and Management Act, Cap. 569) ambayo ilikuwa ni miongoni mwa Sheria kumi zilizofutwa na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 (kwa mujibu wa kifungu cha 189 na Jedwali la Pili la Sheria hiyo).

SHERIA ZINAZOTAMBUA UMUHIMU WA ARDHI YA KILIMO..


Sheria nyingine zilizofutwa na Sheria ya Ardhi zilikuwa ni

Sheria ya Mipango ya Ardhi ya Vijiji (Rural Lands (Planning and Utilization) Act, 1973 Act. 14 of 1973) ambayo kwa mujibu wa kifungu cha 4 na 5, ilimpa mamlaka Rais kupitia amri (order) kutangaza eneo lolote ndani ya Tanganyika kuwa ni eneo maalumu kwa ajili ya kuliendeleza ikiwemo kuweka Kanuni za kusimamia uendelezaji ardhi ya kilimo katika eneo husika (regulating farming operations). Sheria hii iliweka pia adhabu ya kifungo kisichozidi miaka miwili jela kwa mtu atakaekiuka kanuni za kuendeleza ardhi.

SHERIA ZINAZOTAMBUA UMUHIMU WA ARDHI YA KILIMO..


Sheria ya Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo ya mwaka,

2010: imeeleza katika kifungu cha 16 kuwa , ardhi ya nyanda za malisho itatendwa au kut- ambuliwa (demarcated or delineated) kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji na Sheria ya Mipango ya Ardhi (theVillage Land Act and the Land Use Planning Act). Sheria imeyapa mamlaka Mabaraza ya Vijiji kutenga ardhi ya jumuiya katika kijiji ili itumike kwa malisho. Hata hivyo, Sheria hii haina makali ya kulazimisha Mamlaka zinazohusika kutenga ardhi hiyo ya malisho na wala haiweki sifa kamili za ardhi ya Nyanda za malisho. Kwa kuzingatia sifa za wafugaji wengi wa Tanzania, inahitaji kuwepo kwa ardhi ya kilimo miongoni wa wafugaji ili kuwawezesha wafugaji wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji kwa pamoja (mixed farming) kupata ardhi kwa ajili ya kuzalisha mazao.

UMUHIMU WA KUWA NA SHERIA YA ARDHI YA KILIMO

Matokeo ya kuwa na Sheria ya Ardhi ya Kilimo ni: - Kuimarika kwa mfumo wa usimamizi wa kilimo na

matumizi endelevu ya rasimali za kilimo ikiwemo rasilimali ardhi yeyewe, maji, uoto wa asili na mazingira; - Kutambua maeneo yanayofaa kwa kilimo hivyo, huduma zote za kilimo kama vile ugani, pembejeo, zana za kilimo, masoko nk kuelekezwa kwenye maeneo yanayoweza kuleta tija - Kuongezeka kasi ya uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo - Kupungua kwa migogoro inayohusu matumizi ya rasilimali za kilimo ikiwemo ardhi na maji kwa kuwa rasiliamli hizo zitakuwa katika maeneo yanayotambulika kisheria.

UMUHIMU WA KUWA NA SHERIA YA ARDHI YA KILIMO


Umuhimu wa Sheria hii ni: - Kuongezeka kwa uzalishaji, tija na kipato cha mkulima na -

Taifa kwa ujumla. Kuongezeka mchango wa sekta ya kilimo katika kufikia malengo ya Milenia, MKUKUTA, na mipango mingine ya maendeleo nchini Kupungua kwa uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na matumizi endelevu na yenye ufanisi ya rasilimali za ardhi na maji. Kuongezeka uwajibikaji kwa wamiliki wa ardhi ya kilimo na ardhi ya umwagiliaji. Kupanuka kwa masoko ya zana na mashine za kilimo sanjarii na kupungua kwa zana na mashine za kilimo zisizo na ubora

ATHARI ZA KUTOKUWA NA SHERIA YA KULINDA ARDHI YA KILIMO


Kuendelea kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara baina ya watumiaji wa rasilimali ardhi; Uzalishaji wa mazao usio na tija; Ardhi inayofaa kwa kilimo kutumika kwa matumizi yasiyo na manufaa kwa taifa Huduma za kilimo kuelekezwa maeneo ambayo pengine hayana matokeo sahihi. Ardhi ya kilimo kupotea kutokana na kukua kwa shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo makazi nk. Uharibifu wa mazingira kutokana na kukosa usimamizi wa ardhi hivyo kuweza kusabaisha ardhi kutoweka.

ATHARI ZA KUTOKUWA NA SHERIA YA KULINDA ARDHI YA KILIMO..


Kushindwa kutekelezwa kikamilifu kwa Sera, Mipango na

mikakati ya maendeleo kama vile ASDP, KILIMO KWANZA, SAGCOT nk ambayo inahitaji kuwa na ardhi ya kutosha na yenye kuwezesha uzalishaji na shughuli nyingine za maendeleo katika kilimo. Kutotekelezwa kwa dhana ya kuwa na ardhi ya hifadhi (Land Bank) kwa ajili ya kilimo. Kushuka kwa tija kwenye uzalishaji kutokana na wakulima kutumia maeneo madogo ya ardhi na pengine yasiyofaa kwa kilimo husika. Kukosekana kwa mipango sahihi ya uzalishaji

YATAKAYOZINGATIWA KWENYE SHERIA YA ARDHI YA KILIMO


Sheria inayopendekezwa inatarajia izingatie masuala yafuatayo: - Kumpa dhamana Waziri husika kutangaza ardhi ya kilimo - Kuweka kanuni zitakaziotumika kuitambua, kuaainisha, kupima, kuitenga, kusajili na kuitambua kitaaluma madaraja, uwezo na sifa za kila daraja la ardhi ya kilimo; - kuweka masharti ya kusimamia uendelezaji wa ardhi ya kilimo, kuaainisha majukumu ya mmiliki ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa kuwataka wawekezaji na wanaomiliki ardhi ya kilimo kutumia kwa shughuli za kilimo kwa kuzingatia matumizi bora na endelevu.

HITIMISHO
Ongezeko la idadi ya watu linaloenda sambamba na ongezeko la mahitaji ya chakula na mahitaji mengine ya kiuchumi Sheria ya kulinda na kuainisha matumizi endelevu ya rasilimali za kilimo ni muhimu. Katika Kutekeleza azima ya kuwa na Sheria: - Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imekwisha andaa Mapendekezo ya Waraka wa Baraza la Mawaziri (WBLM) - Tarehe 29 na 30 Agosti 2013 Wizara iliitisha mkutano

wa kujadili Mapendelkezo ya Sheria ya kulinda na kuendeleza ardhi ya kilimo uliofanyika mkoani Morogoro. Matarajio ni kuwa na sheria hiyo kabla ya mwishoni mwa mwaka 2014. =ASANTENI KWA USIKIVU =

Vous aimerez peut-être aussi