Vous êtes sur la page 1sur 27

1

MAELEZO YA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CUF,


MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, KWENYE MKUTANO NA
WAANDISHI WA HABARI SERENA HOTEL, DAR ES SALAAM,
TAREHE 11 JANUARI, 2016
KIINI CHA MZOZO WA KIKATIBA NA KISHERIA ZANZIBAR
ULIOTOKANA NA KUFUTWA ISIVYO HALALI KWA UCHAGUZI
MKUU, CHANGAMOTO ZAKE NA NAMNA YA KUUTATUA
Ndugu zangu Waandishi wa Habari,
Awali ya yote, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu
Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya na tukaweza kukutana
hapa asubuhi hii ya leo. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa
kuijaalia nchi yetu kuendelea kubaki katika hali ya amani na utulivu licha
ya changamoto nyingi zinazotukabili. Tunapoona watu wa nchi nyengine,
zikiwemo nchi jirani, wanateseka kwa kukosa amani ndipo tunapozidi
kutambua umuhimu wa neema hii ya amani katika nchi yetu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu na watu
wake na atujaalie hekima na busara katika kuendesha mambo yetu ili
tuendelee kuitunza neema hii aliyotupa.
Pili, nichukue fursa hii kukushukuruni nyinyi wahariri na waandishi wa
habari kwa kuitikia wito wetu na kuja kutusikiliza. Naamini mtatusikiliza
kwa makini, hususan kutokana na uzito wa suala tulilowaitia, na kisha
mtawafikishia Watanzania yale ambayo tumekuja kuwaeleza.
Tumewaita leo hii ili kuzungumzia kwa kina suala la Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matukio yaliyofuata, ikiwemo
hatua isiyo halali kikatiba na kisheria ya Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, kudai kwamba amefuta
uchaguzi huo na matokeo yake, mgogoro uliosababishwa na kitendo
hicho haramu, mazungumzo yanayoendelea kutafuta ufumbuzi wa suala

hilo, pamoja na njama za kuhujumu jitihada zinazoendelea za kutafuta


ufumbuzi kwa njia ya amani.
Naomba mnivumilie wakati nasoma maelezo haya niliyoyaandaa kwani
kwa faida yenu na kwa faida ya Watanzania nimeona kuna haja ya kutoa
maelezo ya kina kidogo ili suala hili liweze kufahamika kwa ukamilifu
wake.
1. UTANGULIZI
Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum
Jecha kutoa tamko lisilo halali kikatiba na kisheria la kuufuta Uchaguzi
Mkuu wa Zanzibar pamoja na matokeo yake kumeitumbukiza Zanzibar
katika mzozo mkubwa wa kikatiba na kisheria. Aidha, kitendo hicho
kimeifedhehesha sana Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mbele ya Jumuiya za kikanda na kimataifa. Mzozo huo pia umeiweka
Zanzibar katika njia panda sio tu kwa hali ya sasa lakini kwa mustakbala
wake wa baadaye na kuirejesha nyuma sana katika jitihada za kujenga
umoja wa kitaifa unaozingatia misingi ya utawala wa sheria, demokrasia
na mfumo wa utawala bora.
Kubwa zaidi, mzozo huo umeleta fadhaa kubwa sana kwa wananchi wa
mirengu yote ya kisiasa. Uchumi na ustawi wa Zanzibar nao umeathirika
sana. Wananchi wako taaban huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu na
bidhaa zikipanda bei kwa kasi wakati mzunguko wa fedha ukiwa
umepotea.
Katika hali hii, hapana budi juhudi za kuutatua mzozo huu zikamilishwe
kwa haraka kwa kuzingatia misingi ya kikatiba, kisheria na pia
mustakbala utaowafanya wananchi wa Zanzibar waamini kwamba
mfumo uliopo wa kikatiba, kiutawala na kisheria ambao umechukua
muda kuujenga unaweza kufanya kazi na pale penye kasoro unaweza
kuimarishwa hatua kwa hatua kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa
miaka kadhaa sasa.
2. YALIYOJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI

1) Hali ya Uchaguzi
Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kama
zilivyo chaguzi nyengine unakwenda sambamba na Uchaguzi Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chaguzi hizo mbili zinafanyika
katika vituo sawa kwa kutumia utaratibu, ulinzi na usimamizi ulio sawa.
Kwa hivyo, siku ya uchaguzi mkuu mwananchi wa Zanzibar ndani ya
kituo kimoja anapiga kura tano (5) badala ya tatu (3) anazopiga
mwananchi aliyepo Tanzania Bara. Kura ambayo mwananchi wa
Zanzibar anapiga ni:
a)
b)
c)
d)
e)

Kura ya Rais wa Zanzibar;


Kura ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
Kura ya Diwani;
Kura ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na
Kura ya Mbunge

Kwa jumla uchaguzi ulifanyika katia njia ya amani, utulivu na bila ya


kutokea vurugu. Waangalizi wa uchaguzi wa ndani na wa nje ya nchi katika
taarifa zao za awali walisifu na kupongeza jinsi uchaguzi ulivyofanyika.
2) Kutangazwa Matokeo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
na Madiwani
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Namba 11 ya 1984, kama
ilivyo kwa Sheria ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
matokeo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani unatangazwa
na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo husika (Returning Officer). Kifungu
cha 88 cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza kama ifuatavyo:
baada ya matokeo ya uchaguzi kuthibitishwa Msimamizi wa Uchaguzi:
(a) Atamtangaza mgombea aliyepata kura nyingi mshindi hapo hapo;
(b) Atampatia aliyechaguliwa taarifa ya kuchaguliwa kwa maandishi;
(c) Atatuma taarifa ya uchaguzi kwa Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya
kuchapishwa katika Gazeti rasmi la Serikali.
Kifungu cha 123 cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza wazi kuwa uchaguzi wa
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi hautahojiwa isipokuwa kwa njia ya Kesi
ya Uchaguzi mbele ya Mahkama Kuu. Kifungu cha 116 cha Sheria ya
Uchaguzi kinaeleza watu ambao wana haki ya kufungua Kesi ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume wala Tume yenyewe haimo katika orodha ya

wanaoruhusiwa kufungua kesi ya uchaguzi kuhoji matokeo ya uchaguzi


yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi.
3) Kukamilika kwa Uchaguzi wa Wawakilishi na Madiwani
Hadi kufikia asubuhi ya tarehe 26 Oktoba, matokeo ya majimbo yote 53
ambayo yalifanya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
yalitangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi na kuwapatia shahada za
kuchaguliwa wale wote walioshinda. Aidha, uchaguzi wa madiwani
ulikamilika na kupatiwa shahada katika Wadi zote zilizofanya uchaguzi.
Kwa maana hiyo, kufikia tarehe 26 Oktoba, uchaguzi wa Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulishakamilika. Aidha, uchaguzi wa
Wabunge nao ulishakamilika na washindi kukabidhiwa vyeti vyao vya kuwa
wamechaguliwa.
Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, kifungu cha 123 kimeeleza wazi kwamba
baada ya uchaguzi kukamilika, unaweza kuhojiwa tu kwa njia ya Kesi ya
Uchaguzi sio vyenginevyo.
4) Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar
Hadi kufikia tarehe 26 Oktoba, asubuhi kazi ya kuhesabu kura za urais na
kukusanya matokeo katika Majimbo yote ya Zanzibar ilishakamilika. Sheria
ya Uchaguzi kifungu cha 42 kinaelekeza ifuatavyo:
Baada ya kukamilika kuhesabu kura katika vituo vyote vya uchaguzi
katika jimbo (na ikihitajika kazi ya kuhesabu tena kura) Msimamizi wa
Uchaguzi wa Jimbo atawasilisha kwa Tume ya Uchaguzi na kwa
mgombea urais au wakala wake:
a) Idadi ya kura za urais zilizopigwa katika Jimbo;
b) Idadi ya kura alizopata kila mgombea;
c) Kama mgombea urais ni mmoja tu idadi ya kura zilizomchagua

Baada ya hapo Tume itajumlisha kura zote za Urais kutoka kila Jimbo.
Sheria ya Uchaguzi, kifungu cha 42(2) inaeleza kwamba Tume inaweza,
ikiwa itakuwa na sababu za msingi, kabla ya kutangaza matokeo kuagiza
kura katika majimbo au jimbo fulani kuhesabiwa upya.
Baada ya kujumuisha matokeo ya urais kutoka katika Majimbo, Sheria ya
Uchaguzi kifungu cha 42(3) kinaelekeza kwamba Tume itamtangaza
mshindi.
Tume ilifanya kazi ya kujumlisha matokeo ya Urais kutoka katika Majimbo
kama inavyoagizwa na Sheria. Baada ya majumuisho hayo, hakuna pahala
ambapo Tume iliagiza kura zihesabiwe upya kama Sheria inavyoagiza ikiwa
kutakuwa na sababu ya kufanya hivyo. Bila ya shaka kwa vile hakukuwa na
kasoro iliyopelekea haja ya kuhesabiwa upya Tume haikuchukua hatua hiyo.
Hadi kufikia tarehe 28 Oktoba, Tume ilishatangaza matokeo ya kura za
Urais kutoka katika majimbo 31; na ilishakamilisha kujumlisha matokeo ya
majimbo mengine 9 (ambayo ilikuwa bado haijayatangaza). Kwa maana
hiyo, kazi ya kujumlisha na kuhakiki matokeo ya majimbo 40 kati ya
majimbo 54 ilikuwa imeshakamilika. Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi
kifungu cha 42(6) Tume inatakiwa itangaze matokeo ndani ya siku 3 tokea
siku ya kupiga kura. Hivyo, tarehe 28 Oktoba ilikuwa ndiyo siku ya mwisho
ambayo Tume ilitakiwa itangaze matokeo ya Urais.
Hata hivyo, majumuisho ya matokeo ya Urais kupitia taarifa ambayo Tume
iliwapatia mawakala wa wagombea au wagombea wenyewe chini ya kifungu
cha 42(1) cha Sheria ya Uchaguzi baada ya kujumuishwa yalikuwa
yanaonyesha kwa ufupi kama ifuatavyo:

MGOMBEA KURA ZA
MGOMBEA
DR. ALI
182,011
MOHAME
D SHEIN
MAALIM
207,847

ASILIMIA
46.28%

52.84%

SEIF
SHARIF
HAMAD
IDADI YA
KURA HALALI

393, 323

Hapa hatukuorodhesha matokeo ya wagombea wengine kwani hakuna hata


mmoja aliyefikisha angalau asilimia 1 ya kura zilizopigwa.
3. KUFUTWA KWA UCHAGUZI NA MWENYEKITI WA TUME
1) Mwenendo wa Mwenyekiti wa Tume na Yaliyojitokeza kabla
ya Kufuta Uchaguzi
Kabla ya Mwenyekiti wa Tume kutoa tamko lake peke yake la kufuta
uchaguzi alionesha dhahiri kuwa alikuwa na ajenda ya siri. Kwanza,
alichelewesha kwa makusudi zoezi la kujumuisha matokeo kwa visingizio
mbali mbali ikiwemo kuchelewa kufika kwenye kituo cha majumuisho
kilichokuwepo Hoteli ya Bwawani, kuondoka mapema na kusingizia
anaumwa. Kwa mfano siku ya tarehe 27 Oktoba aliahirisha zoezi hilo kwa
madai ya kuwa na tatizo la sindikizo la damu. Siku ya tarehe 28 Oktoba
ambayo kwa mujibu wa Sheria ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kutangaza
matokeo, Mwenyekiti hakuonekana kabisa katika kituo cha kutangaza
matokeo katika Hoteli ya Bwawani. Baada ya Wajumbe waliobaki wa Tume
kuona wanachelewa na siku hiyo ilikuwa ya mwisho, waliamua kwamba
Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Abdulhakim Ameir Isssa aendelee
kuongoza Tume kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya Urais kwa vile
kifungu cha 119(10) cha Katiba ya Zanzibar kinaruhusu kufanya hivyo.
Wakati zoezi hilo likiendelea mambo matatu makubwa yalijitokeza:
a) Kituo cha Bwawani kilizingirwa na Jeshi la Ulinzi la Tanzania
(JWTZ) wakitoa amri ya kuzuia kila aliyekuwemo ndani asitoke na
aliyekuwa nje asiingie katika eneo hilo;
b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Abdulhakim Ameir
Issa alipewa taarifa ya wito muhimu na mmoja wa watumishi wa

Tume na alipotoka nje ya ukumbi wa kikao cha Tume alichukuliwa na


askari Polisi na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kilimani;
c) Televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na redio ya
Shirika hilo yalitoa matangazo ya tangazo la Mwenyekiti wa Tume
kufuta uchaguzi na matokeo yake;
Baada ya hapo Tume haikuitishwa tena hadi tarehe 1 Novemba, 2015
ambapo Mwenyekiti aliwaarifu Wajumbe wa Tume yafuatayo:
i.

ii.

Kwanza alitangulia kuomba radhi Wajumbe kwa vile baada ya


kukutana na vyombo (bila ya kutaja vyombo gani) alilazimika
kusema baadhi ya mambo ya uongo katika taarifa yake na kufuta
uchaguzi ili kuokoa hali;
Alitaka Wajumbe wamuunge mkono kwa kitendo alichofanya;

Tarehe 12 Novemba, Mwenyekiti wa Tume alitoa Tangazo rasmi Namba 130


la kufuta uchaguzi (matokeo) kupitia Gazeti Rasmi la Serikali
lililochapishwa tarehe 6 Novemba. Hata hivyo, Tangazo hilo lilikuwa na
kasoro za wazi za kisheria ambazo nitazieleza hapo mbele.
2) Uhalali wa Mwenyekiti wa Tume kufuta Uchaguzi
Mbali ya kwamba kitendo cha Mwenyekiti wa Tume kimedhihirika kuwa ni
njama za wazi za kisiasa ambazo zilipangwa na kutekelezwa na Mwenyekiti
wa Tume, vyombo vya ulinzi na viongozi wa kisiasa ambao sasa
wanamtetea, uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume kufuta uchaguzi hauna
uhalali wowote kwa sababu zifuatazo:
a) Uchaguzi Kukamilika: Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi na Madiwani kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi
ulishakamilika. Kwa upande wa uchaguzi wa Rais nao
ulishakamilika isipokuwa hatua ya kutangaza matokeo ambayo
nayo kwa mujibu wa sheria ilitakiwa iwe imeshakamilika.
Kama ilichelewa ilicheleweshwa makusudi na Mwenyekiti
katika juhudi zake za kutafuta visingizio vya kuharibu uchaguzi
ili mshindi halali asitangazwe. Tume haina mamlaka ya

kuahirisha, kutengua matokeo au kufuta uchaguzi uliokwisha


kamilika. SHERIA YA UCHAGUZI imeeleza wazi mamlaka
ya Tume baada ya kazi ya kuhesabu kura kukamilika. Mamlaka
pekee ni ya kurudia kuhesabu kura kwa majimbo yote au kwa
Jimbo moja iwapo itaridhika kwamba ipo sababu ya msingi ya
kufanya hivyo. Kifungu cha 42(2) cha Sheria ya Uchaguzi
imeeleza wazi juu ya uwezo huo wa Tume. Kuipa mamlaka
Tume kutengua uchaguzi uliokwisha kamilika ni sawa na
kuingilia kazi za mhimili wa Mahkama. Hata Mahkama
yenyewe inafungwa na Sheria ya Uchaguzi. Kifungu cha 123
kimeeleza watu ambao wanaweza kuhoji matokeo ya uchaguzi
baada ya kutangazwa na Returning Officer. Mwenyekiti wa
Tume au Tume hawamo katika orodha ya wanaoweza kuhoji
uchaguzi baada ya kutangazwa matokeo. Aidha, chini ya
Sheria ya Ukomo, Mahkama haiwezi kusikiliza tu shauri lolote
lazima izingatie muda unaokubalika kusikiliza shauri;
b) Mamlaka ya Mwenyekiti: Ni wazi kuwa Mwenyekiti alivunja
Katiba. Alikwenda kinyume na kifungu cha 119(1) cha Katiba
na alikiuka kifungu cha 119(10) cha Katiba juu ya utaratibu wa
Tume kufanya maamuzi kwa kuamua kufuata uchaguzi bila ya
kuitisha kikao cha Tume wala kushauriana na Tume. Kifungu
cha 119(1) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza muundo wa Tume
ambayo imeshirikisha wadau wakuu wa uchaguzi na watu
wengineo huru. Kifungu cha 119(10) kinaweka utaratibu wa
Tume kufanya maamuzi na kimeeleza kwa maelezo ya wazi
kama ifuatavyo:
kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni
Mwenyekiti au Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wanne
na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na
Wajumbe walio wengi.
Ni dhahiri kuwa Katiba imesisitiza suala la maamuzi ya Tume
kufanywa kwa kupitia vikao na uamuzi kufanywa baada ya
kuungwa mkono na Wajumbe walio wengi. Katiba imetumia
daraja mbili za msisitizo kwa kutumia neno kila (maamuzi
ya Tume) na neno lazima.

Kwa kufanya maamuzi peke yake, Mwenyekiti alipaswa


achukuliwe hatua na Rais ya kusimamishwa, kuchunguzwa na
akipatikana na kosa kufukuzwa chini ya vifungu vya 119(6), (7)
na (8) vya Katiba;
c) Mamlaka ya Tume: Ingawa Mwenyekiti aliitisha kikao tarehe
1 Novemba na kuitaka Tume ihalalishe kitendo chake cha
kufuta matokeo, lakini Tume haina mamlaka ya kuhalalisha
kitendo chochote kinachokiuka Katiba au Sheria. Tume
ingeweza kuhalalisha jambo ambalo kwanza Mwenyekiti
mwenyewe ana mamlaka nalo na Tume ina mamlaka nalo
kulifanya lakini pengine taratibu tu hazikukamilika. Kwa vile
Tume haina mamlaka ya kuhalalisha jambo ambalo ni kinyume
na Katiba na Sheria, kitendo cha Tume kutaka kuhalalisha
kitendo cha Mwenyekiti cha kufuta uchaguzi uliokwisha
kamilika ni batili;
d) Udanganyifu na Ubatili wa Tangazo Rasmi la Kufuta
Uchaguzi: Kama nilivyotangulia kueleza kwamba tarehe 6
Novemba, Mwenyekiti wa Tume alitoa Tangazo Namba 130
katika Gazeti rasmi la Serikali kufuta uchaguzi. Tangazo hilo
lina udanganyifu wa wazi na kasoro nyengine kadhaa za
kisheria kama ifuatavyo:
Udanganyifu: Tangazo linaeleza kwamba ni uamuzi wa
Tume ya Uchaguzi uliofanywa tarehe 28 Oktoba. Kuna
ushahidi usio na shaka kwamba tarehe 28 Oktoba, Tume
ya Uchaguzi haikukutana kabisa hata kwa njia isiyo
rasmi kwa vile Mwenyekiti hakwenda katika kituo cha
kutoa matokeo ya uchaguzi seuze kukutana rasmi kwa
mujibu wa Katiba na kutoa maamuzi kama Katiba
inavyoelekeza;
Migongano: Tamko la Mwenyekiti alilolitoa tarehe 28
Oktoba kupitia vyombo vya habari vya ZBC lilieleza
wazi kuwa anafuta uchaguzi na matokeo yake yote.
Hata hivyo, Tangazo katika Gazeti Rasmi linaeleza kuwa
amefuta matokeo ya uchaguzi. Huu ni mgongano
mkubwa ambao una maswali mengi bila majibu;

10

Uhalali wa kisheria: Katika Tangazo la Kisheria namba


130, Mwenyekiti amenukuu vifungu vya Katiba na
Sheria anavyodai vinampa uwezo kufuta Uchaguzi.
Vifungu vyote alivyonukuu sio tu kwamba
havizungumzii mamlaka ya kufuta uchaguzi lakini pia
havitoi uwezo kwa Tume kufanya hivyo. Amenukuu
kifungu cha 119(10) cha Katiba ambacho kinaeleza tu
akidi ya vikao vya Tume na kwamba lazima maamuzi
yote ya Tume yaungwe mkono na Wajumbe walio wengi.
Amenukuu kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchaguzi
ambacho kinazungumzia utaratibu wa kutoa matangazo
ambayo Tume kisheria ina mamlaka kuyatoa na
amenukuu kifungu cha 5 cha Sheria ya Uchaguzi
ambacho kinazungumzia kazi za Tume na sio mamlaka
ya Tume. Ni dhahiri vifungu hivyo vimenukuliwa kwa
ubabaishaji kwa nia ya kupotosha kwamba Tume inao
uwezo wa kufuta uchaguzi.
e) Hoja ya Kasoro katika Uchaguzi: Hoja inayotumika kuwa
uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi lazima izingatiwe kwa
makini. Kwanza, Sheria yenyewe ya Uchaguzi imetoa
utaratibu wa kufuatwa endapo kuna malalamiko ya ukiukwaji
wa taratibu za uchaguzi. Kwa mfano, kifungu cha 74 kinaweka
utaratibu wa kufunga kituo iwapo itajitokeza fujo katika kituo
cha uchaguzi. Vifungu vya 71, 76, 80B na 85 vinaelekeza kwa
ufasaha namna ya kushughulikia kasoro mbali mbali
zitazojitokeza katika uchaguzi. Sheria imetoa fursa za wazi
kwa mwenye malalamiko kuyawasilisha kwa kupitia fomu
maalum. Kujaza fomu hizo ni sharti la msingi katika kuyafanya
malalamiko kuwa halali. Ingawa hazikufuata taratibu,
malalamiko yaliyowasilishwa na CCM kwa barua yalijadiliwa
na Tume na kutupiliwa mbali kwa kauli moja. Hivyo, kwa
mujibu wa Sheria hapakuwa na malalamiko yaliyowasilishwa
mbele ya Tume. Mwenyekiti wa Tume alibuni mwenyewe
kasoro na kuzitolea uamuzi yeye mwenyewe na peke yake.
Aidha, tokea chaguzi za vyama vingi zianze zimekua na kasoro.
Kasoro kubwa kuliko zote ilitokea katika uchaguzi wa mwaka

11

2000 ambapo majimbo 16 ya Mkoa wa Mjini Magharibi ilibidi


yarudie uchaguzi. Pamoja na kasoro hizo chaguzi
zilikamilishwa na Serikali kuundwa. Kasoro kwa kawaida
zilishughulikiwa baadaye kwa kurekebisha Sheria na hata
Katiba ili chaguzi zinazofuata ziwe bora zaidi. Suala la
kujiuliza kuwa kasoro za mara hii ambazo hazikuwasilishwa
kwa taratibu zinazofaa zilikuwa kubwa kiasi gani (were the
irregularities so fatal to the election process?). Hivi kweli
Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa na kasoro nyingi kuliko hata
ule wa mwaka 2000? Uchaguzi hauwezi tu kurejewa bila
kufanyika uchunguzi huru na wa kitaalamu usiokuwa na
maslahi ya kisiasa au kuficha ukweli;
f) Tume Kuingiliwa Katika Kazi zake: Kwa mujibu wa kifungu
cha 119(12), Tume haipaswi kupokea maagizo au kufuata
maagizo ya chombo au chama chochote cha siasa. Ni dhahiri
kwamba uamuzi wa Mwenyekiti, kama yeye mwenyewe
alivyowaeleza Makamishna wenziwe tarehe 1 Novemba,
umetokana na kufuata maagizo ya vyombo, maagizo ya Chama
na amri ya Serikali. Aidha, kitendo cha Makamu Mwenyekiti
wa Tume kukamatwa na kupelekwa Polisi wakati anatekeleza
majukumu yake ni ukiukwaji uliochupa mpaka wa Katiba na
pia ni kuingilia kazi za Tume kwa uwazi kabisa;
Athari ya mambo yote haya ni ukiukwaji mkubwa na wa wazi wa Katiba
ambao hauwezi kutetewa au kuhalalishwa kwa kutambua ufutwaji usio
halali wa uchaguzi unaodaiwa kufanywa na Mwenyekiti wa Tume.
4. ATHARI NA CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA KUFUTWA
KWA UCHAGUZI
Kufutwa kusiko halali kwa uchaguzi kumepelekea kuwepo athari kadhaa za
kikatiba, kisiasa na kijamii. Miongoni mwa athari kubwa ni kama zifuatazo:
1) Mgogoro Mkubwa wa Kikatiba na Kisheria
a) Kutokuwepo Rais Halali wa Zanzibar

12

Mgogoro wa kikatiba ulioikumba Zanzibar kutokana na kufutwa kusiko


halali kwa uchaguzi una nyanja nyingi. Ya kwanza ni suala la Rais kumaliza
muda wake kikatiba. Katiba ya Zanzibar chini ya kifungu cha 28(2)
kimeeleza wazi kwamba muda wa Rais kushikilia wadhifa huo ni miaka
mitano. Kifungu cha 29 kinaeleza masharti ya kuongeza muda huo wa
miaka mitano ambayo ni magumu na yenye ukomo maalum. Hata hivyo,
washauri wa Rais kwa kutumia tafsiri isiyo sahihi ya Katiba wamemshauri
kwamba kwa kutumia kifungu cha 28(1)(a) anaweza kuendelea kuwa Rais
hadi Rais mpya atapoapishwa. Kwa ufupi tunaangalia athari ya tafsiri hiyo:
Mipaka ya Kifungu cha 28(1)(a)
Kifungu cha 28(1)(a) kinachoruhusu Rais aendelee mpaka Rais
anayefuata ale kiapo kina mipaka ya wazi katika Katiba. Mpaka wa
kwanza unahusu muda wa Urais. Katiba chini ya kifungu cha 28(2)
kimeweka bayana kuwa muda wa Urais ni miaka mitano. Hili ni sharti
mahsusi na ndio maana Katiba haijaruhusu suala la kuongezwa muda wa
miaka 5 lifanywe kiholela au kwa mlango wa nyuma. Kifungu cha 29
cha Katiba kimeweka bayana sababu na utaratibu wa kuongeza miaka
mitano. Sababu hizo ni nzito na muda kuongezwa ni mahsusi. Kifungu
cha 29 kinaeleza: ikiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imo
katika vita na ikiwa Rais anaona kuwa ni muhimu kuzuia uchaguzi,
Baraza la Wawakilishi linaweza kwa kupitisha azimio, kuzidisha muda
wa miaka mitano uliotajwa kwenye kijifungu cha (2) cha kifungu cha
28 katika kipindi hadi kipindi lakini hakuna kipindi kitachozidi miezi
sita mfululizo.
Mpaka wa pili unaoonesha ni kwa kiasi gani Katiba haitoi mwanya wa
kujiongezea miaka mitano, ni ile ya ukomo wa vipindi viwili vya miaka
mitano chini ya kifungu cha 30(1)(b). Katika kuonesha jinsi Katiba
ilivyo strict katika ukomo wa miaka mitano, tafsiri ya miaka mitano chini
ya kifungu cha 34(iv) imefanywa kwa namna ambayo Katiba inaruhusu
miaka mitano ipungue kuliko kuzidi. Kifungu hicho kinaeleza: bila
kujali masharti ya vifungu vya 28(3) na 30(1) (b) vya Katiba, endapo
mtu anayemfuata Rais kwa madaraka atashika kiti cha Rais kwa
kipindi kinachopungua miaka minne ataruhusiwa kugombea nafasi ya
Rais mara mbili lakini kama atashika kiti cha Rais kwa muda wa

13

miaka minne au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara


moja tu.
Kama Katiba ingekuwa imelichukulia kipindi cha miaka mitano kwa
wepesi kama alivyotaka kutuaminisha aliyetoa ushauri basi isingechukua
shida ya kutafsiri maana ya miaka mitano kwa namna iliyofanywa na
kifungu cha 34(iv).
Hivyo tafsiri yoyote ya Katiba inayotoa mwanya wa kuongeza kipindi
cha Urais cha miaka mitano kwa njia nyepesi, ya kiholela na ya kiujanja,
tafsiri hiyo haiwezi kuwa sahihi. Katika kutafsiri Katiba Profesa Crabe
ametoa angalizo muhimu kwa kusema kuwa: its [the constitution]
provisions are not mere rules of conduct for the guidance of society,
but also commands to be obeyed. It is not an equation in mathematics
to be interpreted by reference to numbers, it is, in a sense, organic.all
the duties, obligations, powers, privileges and rights must be exercised
in accordance with the letter of the constitution. More than that, they
should be exercised and enforced in accordance with the spirit of the
constitution
Mgongano wa Tafsiri na Kifungu cha 28(2) na 29
Ushahidi mwengine wa wazi kuwa tafsiri inayotolewa ya kifungu cha
28(1) (a) kuwa sio sahihi ipo katika Kanuni za tafsiri ya sheria. Moja ya
Kanuni za msingi ni kuwa tafsiri yoyote ya sheria au kifungu cha sheria
inayopelekea kufanya kifungu chengine cha sheria kisiwe na maana
(irrelevant) au kisiwe na haja ya kuwepo (redundant) basi tafsiri hiyo ni
ya kituko (absurd). Na tafsiri yoyote ya kituko basi sio sahihi. Tafsiri
inayotolewa kumruhusu Rais aendelee inakifanya kifungu cha 28(2)
kinachoweka muda wa Urais kuwa miaka mitano kisiwe na maana.
Aidha, inakifanya kifungu cha 29 cha Katiba kinachoeleza sababu na
utaratibu wa kuongeza huo muda wa miaka mitano kisiwe na haja ya
kuwepo. Lakini pia inafanya mfumo mzima wa kuvunjwa Baraza la
Wawakilishi na kuitishwa uchaguzi mkuu ndani ya muda maalum na
muda wa ukomo wa vipindi vya Urais vyote visiwe na maana. Kifungu
cha 28(1) (a) hakizungumzii muda wa Urais bali kinazungumzia wakati tu
mahsusi ndani ya hiyo miaka mitano ambapo kiti cha Rais atakabidhiwa
mtu mwengine.

14

Kifungu hicho kinaweza tu kutumika kuongezeka kwa miaka mitano


iwapo itatokea dharura halali kwa mujibu wa sheria (exigency by
operation of the law) kama vile Uchaguzi katika jimbo au majimbo fulani
unapotokea kuharibika kwa sababu inayokubalika na ambayo sheria
imeiruhusu Tume kuakhirisha uchaguzi na kuitisha siku nyengine. Hii ni
dharura ambayo sheria imeshaiwekea misingi yake. Au dharura
isiyotazamiwa na inayokubalika (unforeseeable legitimate exigency).
Mfano mzuri hapa ni pale mgombea anapofariki kabla tu ya uchaguzi au
kabla ya kuapishwa. Hizi ni dharura ambazo mifumo yote ya kisheria
inazitambua na hata Mahkama imezitambua.
Athari za Tafsiri isiyokuwa sahihi
Tafsiri isiyo sahihi iliyotolewa ina athari kubwa zifuatazo:
Kwanza, Katiba haikuweka muda maalumu wa kufanya uchaguzi
uliofutwa katika mazingira yasiyokuwa halali. Kisheria uchaguzi
uliofutwa katika mazingira hayo hauitwi kwamba ni uchaguzi
uliofutwa bali ni uchaguzi unaodaiwa umefutwa (purported
nullification of election). Katiba imeweka muda kwa chaguzi
zinazoitishwa kihalali tu ama kwa kuvunjwa Baraza, kufariki
mwenye wadhifa au matokeo kulingana. Kwa tafsiri iliyotolewa ina
maana kuwa Rais aliyepo anaweza kushika wadhifa huo hadi Tume
ya Uchaguzi itapoamua kuitisha uchaguzi. Kwa vile hakuna ukomo
wala muda maalum uliowekwa ndani ya Katiba wala Sheria
uchaguzi unaweza kuitishwa hata baada ya mwaka mmoja au miwili
kwa vile hakuna ukomo wa kikatiba wala wa kisheria. Athari ya
jambo hili ni sawa na kuisimamisha sehemu ya Katiba;
Pili, tafsiri hiyo ya Katiba inatoa mwanya kwa Rais kutosimamia
Katiba kwa kutomchukulia hatua Mjumbe wa Tume aliyekwenda
kinyume na Katiba au sheria iwapo tu Mjumbe huyo amefanya
hivyo kwa manufaa ya Rais. Kifungu cha 119(6) (7) na (8)
vinaeleza wajibu wa Rais kusimamia nidhamu na uadilifu wa Tume.
Kama Rais atafumbia macho wajibu huo kwa vile amefaidika na
uhalifu huo dhidi ya Katiba ni sawa na kusema kuwa Tume ya

15

Uchaguzi ipo juu ya Katiba na Sheria za nchi kwa vile Rais ana hiari
ya kusimamia vifungu vya Katiba vinavyosimamia nidhamu yao.
Kubwa zaidi kuliko yote ni kujiuliza iwapo mwendo huo wa Rais
hauendani kinyume na masharti ya kifungu cha 37(2) cha Katiba
kinachokataza Rais kufanya kitendo kinachokwenda kinyume na
Katiba na kwamba akifanya hivyo anaweza kushitakiwa mbele ya
Baraza la Wawakilishi.
Tafsiri sahihi ni kwamba Rais lazima ashike madaraka ya Urais na aachie
nafasi hiyo ndani ya muda huo wa miaka mitano isipokuwa kwa dharura
halali za kisheria ambazo zinakubalika. Ikiwa ukomo huo hautazingatiwa
basi Katiba yenyewe haitakuwa na maana na masharti yaliyowekwa
bayana tena kwa maandishi yatakuwa pia hayana maana. Aliyewahi
kuwa Jaji Mkuu wa Marekani, Justice John Marshall aliwahi kueleza haja
ya wanaotakiwa kulinda Katiba kutii masharti ya Katiba kwa kueleza
yafuatayo: to what purpose are powers limited, and to what purpose is
that limitation committed to writing, if these limits may, at any time, be
passed by those intended to be restrained? [Marbury v. Madison, pg 137]
Hivyo, mgogoro wa kwanza ni kutokuwepo Rais halali wa Zanzibar tokea
tarehe 3 Novemba, 2015. Pamoja na hali hiyo, anayedai kuendelea na
Urais amekuwa akifanya maamuzi makubwa yakiwemo ya uteuzi ambayo
yana athari kubwa hapo baadaye.
b) Kutokuwepo Mawaziri
Baraza la Wawakilishi tokea tarehe 12 Novemba, limemaliza muda wa
uhai wake kwa mujibu kifungu cha 92(1) cha Katiba. Hali hii ni tofauti
sana na kipindi ambacho Baraza limevunjwa chini ya vifungu vya 90(1)
na 91(1) vya Katiba. Katika Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya
Muungano na takriban katika nchi zote zenye asili ya mfumo wa
Westminster na hata mfumo wa Jamhuri (republican form of government)
zipo dhana mbili kuu kuhusiana na uhai wa Baraza la Wawakilishi
(Bunge). Dhana ya kwanza ni ya Baraza kuvunjwa (dissolution of
parliament) na dhana ya pili ni ile ya Baraza kumaliza muda wake (lapse
of tenure of Parliament). Dhana hizi mbili ni tofauti na zina athari tofauti
katika uhai wa Bunge na wa Serikali. Hata katika Katiba ya Zanzibar ya

16

1984, tokea awali ilipotungwa mwaka 1984 dhana hizi mbili


zilitenganishwa na ziliwekewa masharti tofauti juu ya uhai wa Baraza.
Dhana ya Baraza kuvunjwa na athari zake iliwekwa chini ya kifungu cha
90(1) na ile ya Baraza kumaliza muda iliwekwa chini ya kifungu cha 92
sawa na Katiba ilivyo sasa hivi. Tofauti yao ni neno tu ambalo
limetumika; chini ya Toleo la mwanzo la Katiba neno lililotumika ni
Baraza litapovunjika na Toleo la 2010 neno linalotumika ni Baraza
litapovunjwa. Tofauti hii ya maneno ilifanywa na kifungu cha 25 cha
Sheria ya Marekebisho ya Kumi ya Katiba, Namba 2 ya 2002. Hata
hivyo mabadiliko haya ya maneno hayakubadili dhana hizi mbili kwa
namna yoyote ile.
Katiba ya Zanzibar imeweka dhana mbili katika uhai wa Baraza. Kwanza
Baraza linavunjwa. Madhumuni ya kuvunjwa ni kutoa fursa ya kuandaa
uchaguzi mkuu. Katiba imetoa siku 90 kufanyika maandalizi ya uchaguzi
hadi Baraza na Rais mpya kuapishwa. Katika kipindi hicho ndipo
ambapo Mawaziri wanaendelea kuwa Mawaziri. Kifungu cha 48(b)
kimetumia maneno ya wazi kwamba nafasi ya Waziri itakuwa wazi:
iwapo mjumbe ameacha kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa
sababu nyengine zaidi ya kuvunjika kwa Baraza hilo. Hivyo, Baraza
kumalizika muda (lapse or expiration of tenure) ni wazi haingii katika
dhana ya Baraza kuvunjika (dissolution). Baraza likimalizika muda
linakuwa halipo na ndio maana hata Katiba, kifungu cha 92(1) kimetumia
maneno Maisha ya Baraza la Wawakilishi yataendelea kwa muda wa
miaka mitano. Kwa hivyo baada ya miaka mitano uhai wa Baraza
husika unaisha na kwa hivyo Waziri anakosa sifa ya kuwa Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi. Tafsiri ya Waziri iliyopo katika kifungu cha 134
inaliweka hili bayana zaidi kama ifuatavyo: Waziri maana yake ni
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi
aliyekabidhiwa wadhifa wa kazi ya Waziri katika Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar. Aidha kifungu cha 42(2) na 43(2) vinavyohusu uteuzi wa
Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi vimeeleza wazi kuwa
Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Kwa kuelewa kwamba dhana ya kuvunjwa Bunge (dissolution) na
kumalizika muda au uhai wa Bunge (lapse or expiration of tenure) ni vitu

17

viwili tofauti, ndio maana Katiba ya baadhi ya nchi wameweka bayana


dhana hizi mbili katika suala la kuendelea nafasi ya uwaziri baada ya Bunge
kuvunjwa au kumaliza muda. Katiba ya Fiji kwa mfano, katika kifungu cha
105(2) inaeleza: subject to subsection (2), appointment of a Minister
terminates if;
(a)
(d) the Minister ceases to be a Member of Parliament
(2) if a Minister ceases to be a Member of Parliament because of the expiry
or dissolution of the House of Representatives, he or she continues in office
as Minister until the next appointment of a Prime Minister.
Katiba ya Zanzibar imeruhusu kwa maneno ya wazi kuwa Waziri aendelee
na uwaziri katika kipindi ambacho Baraza limevunjwa tu na sio wakati
ambao Baraza limemaliza muda. Kwa hivyo tokea Baraza kumaliza muda
wake tarehe 12 Novemba, Zanzibar haina mawaziri. Hata hivyo baadhi ya
waliokuwa mawaziri wamefanywa kama bado ni mawaziri na wanaendelea
kufanya maamuzi makubwa jambo ambalo ni la hatari.
c) Kutokuwepo Baraza la Wawakilishi
Baraza la Wawakilishi limemaliza muda tokea tarehe 12 Novemba. Hoja
kuhusu suala hili yameelezwa kwa kina katika aya (b) hapo juu inayohusu
kutokuwepo mawaziri. Aidha, Spika wa Baraza hilo amethibitisha kwamba
Baraza halipo ingawa jambo la kushangaza naye amedai yeye na Naibu
wake wanaendelea kushika madaraka yao mpaka Spika mpya atapoapishwa.
Katiba ya Zanzibar imeeleza wazi chini ya kifungu cha 5A mgawanyo wa
kazi baina ya mihimili mikuu ya Serikali. Miongoni mwa mihimili hiyo ni
Baraza la Wawakilishi. Kazi muhimu ya Baraza ni kuisimamia Serikali.
Kutokuwepo chombo hicho huku Serikali ikiendelea na kazi zake ni jambo
la kuvunja katiba kwa kiasi kikubwa.
2) Hoja ya Kurudiwa Uchaguzi
Hoja ya kurudiwa uchaguzi ambayo imeshikiwa bango na Chama cha
Mapinduzi, Zanzibar ni ya kutafuta manufaa ya kisiasa baada ya Chama cha

18

Mapinduzi kushindwa katika uchaguzi. Mbali ya matokeo ya uchaguzi ya


Urais wa Zanzibar ambayo yanaonyesha wazi kuwa CCM imeshindwa kwa
kura nyingi sana kwa kiwango na uzoefu wa Zanzibar, hata kura za Urais wa
Jamhuri ya Muungano kwa upande wa Zanzibar zinaonyesha hivyo hivyo na
kwa hiyo kuthibitisha kuwa CCM ilipoteza uchaguzi huo. Kwa muhtasari
matokeo ya Urais wa Muungano kwa upande wa Zanzibar ni kama
yafuatavyo:

MGOMBEA
DR. JOHN
POMBE
MAGUFULI
EDWARD
NGOYAYE
LOWASSA

KURA HALALI
194,317

ASILIMIA
46.5%

211,033

50.50%

IDADI YA KURA
HALALI

417,882

Matokeo ya kura za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani yote yanaonyesha


CCM imeshindwa kwa idadi ya kura za walio wengi (popular votes). CCM
imeweza kupata viti sawa na CUF katika uwakilishi na ubunge kwa sababu
ya mbinu zilizotumika katika ukataji wa majimbo.
Hivyo, kimsingi Hoja ya kurudia uchaguzi haina msingi na haiwezekani
kutekelezwa kwa sababu kadhaa. Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na
zifuatazo:
a) Kukosekana Uhalali wa Msingi wa Kurejea Uchaguzi
Kama ilivyoelezwa awali kwamba hatua ya Mwenyekiti wa Tume kufuta
uchaguzi haikuwa halali na ina kasoro nyingi za kikatiba na kisheria.
Kurejea uchaguzi ni sawa na kuhalalisha kitendo batili alichofanya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Aidha ni kuweka precedent mbaya
kwamba uchaguzi unaweza kufutwa kwa sababu zozote zile japo kama
sio halali.
b) Kujenga Msingi Batili Kisheria Katika Mustakbala wa Uchaguzi

19

Kiini cha mzozo uliozushwa katika uchaguzi ni uamuzi batili wa


Mwenyekiti wa Tume. Kurejea uchaguzi bila kupatia ufumbuzi juu ya
uhalali wa uamuzi wa Mwenyekiti ni sawa na kuhalalisha kitendo cha
Mwenyekiti na kutoa ruhusa kuwa huko mbele anaweza kufanya tena
kitendo kama hicho au Tume inaweza kufanya kitendo kama hicho. Hii
ni kujenga msingi wa kuwa na chaguzi zisizokwisha na mizozo isiyo na
mwisho. Lazima mipaka ya Mwenyekiti na Tume iwekwe bayana ili
hapo baadaye ijulikane nini ukomo wa mamlaka yao.
c) Kujenga Imani ya Wapiga Kura
Uchaguzi ni wa wapiga kura na sio wa vyama au wagombea. Lazima
wapiga kura waridhishwe kuwa uchaguzi ulikuwa na tatizo la kiasi cha
kuufanya matokeo yake yasionyeshe dhamira na uamuzi wa wapiga kura.
Hadi sasa hakuna mwelekeo unaonyesha kuna ukweli katika tuhuma za
kasoro za uchaguzi. Moja ya madai ya CCM ni kwamba eti Pemba watu
waliopiga kura walikuwa ni zaidi ya walioandikishwa lakini ukweli ni
kwamba takriban watu 29,000 walioandikishwa hawakupiga kura
kisiwani humo. Katika mazungumzo yanayoendelea Ikulu, Zanzibar
baina ya viongozi, CCM imetakiwa mara kadhaa kuleta ushahidi wa
tuhuma zake kwamba kulikuwa na hujuma lakini imeshindwa kufanya
hivyo. Matamko ya Waangalizi wa Uchaguzi na namna tuhuma za
kasoro za uchaguzi zilivyoibuliwa na Mwenyekiti wa Tume haziwezi
kuwashawishi wapiga kura kwamba kulikuwa na kasoro katika uchaguzi.
Hoja ya kurudiwa uchaguzi inaonekana wazi kuwa ni ajenda ya kisiasa
ya chama kilichoshindwa. Hali hii ni sababu tosha ya kuleta fujo iwapo
hatua yoyote ya kurudia uchaguzi itachukuliwa.
d) Changamoto za Kuunda Tume Mpya ya Uchaguzi
Ni dhahiri kuwa uchaguzi wa Zanzibar umehujumiwa na Mwenyekiti wa
Tume kwa sababu ya sindikizo la kisiasa. Kwa vyovyote vile yeye hafai
tena kuendelea kuiongoza Tume hiyo katika kazi yoyote ya Tume
iliyobaki. Ni lazima akae pembeni.
Kurejea uchaguzi ni sawa na kuihukumu Tume nzima kuwa ina makosa
wakati makosa hayo yalifanywa na mtu mmoja tu. Hivyo, kwa vyovyote
vile, kama uchaguzi utarudiwa, haitawezekana kwa Tume iliyopo na

20

Sekretarieti kusimamia uchaguzi wa marudio. Kufanya hivyo ni


mgongano mkubwa wa maamuzi kwamba Tume iliyokiri kuharibu
uchaguzi isimamie tena uchaguzi wa marudio. Hivyo, kama Tume na
Sekretarieti itabidi iondoke na kuunda Tume na Sekretarieti mpya, bado
kutakuwa na changamoto kubwa zaidi ya kuunda Tume mpya ya
uchaguzi. Miongoni mwa changamoto kubwa ni kama zifuatazo:
i.

Kuondolewa Wajumbe waliopo: kwa mujibu wa kifungu cha


119(6),(7) na (8) cha Katiba, Wajumbe wa Tume wana kinga ya
kutoondolewa katika nafasi yao isipokuwa kwa kufuata
utaratibu maalum sawa na ule wa kumuondoa Jaji wa Mahkama
Kuu (security of tenure). Njia nyengine nyepesi ni kwa
Mjumbe kujiuzulu kwa hiari yake. Hii ni changamoto kubwa
hasa kwa kuzingatia kwamba Wajumbe wanaamini kwamba
hawakufanya makosa yoyote na aliyefanya makosa tena kwa
makusudi anajulikana lakini analindwa kwa maslahi ya kisiasa;

ii.

Utaratibu wa Kuunda Tume ya Uchaguzi; kwa mujibu wa


kifungu cha 119(1)(b) cha Katiba, Wajumbe wawili wa Tume
ya Uchaguzi wanateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya
Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi.
Ni ukweli ulio wazi kwamba sasa hivi Baraza la Wawakilishi
limemaliza muda tokea tarehe 12 Novemba. Kwa sababu hiyo,
hakuna Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Baraza ambalo
halipo. Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Baraza
lililopita, tukiweka siasa upande, kisheria, ni dhahiri kuwa
amesita kuwa na wadhifa huo kwa vile Baraza limemaliza
muda chini ya masharti ya kifungu cha 92(1) cha Katiba. Kabla
ya Baraza kumaliza muda wake, ni wazi kuwa alikuwa
akilindwa na kifungu cha 48(b). Baada ya Baraza kumaliza
muda wa uhai wake, kifungu hicho hakiwezi kutumika. Aidha
kifungu cha 48(d) ambacho baadhi ya watu wanadhani
kinaweza kutumika hakiwezi kutumika kwa vile masharti ya
aya za (a) mpaka (d) ya kifungu cha 48 ni ya kujitosheleza kila
moja ndio mana ikatumika neno au baina ya kila aya. Hivyo
kwa vile Kiongozi wa shughuli za Serikali katika Baraza
lililomaliza muda wake amesita kuwa Mjumbe wa Baraza kwa

21

sababu ya Baraza kumaliza uhai wake, hawezi kutumia


masharti ya kifungu cha 48(d) kwa vile tayari ameshaondokewa
na sifa chini ya kifungu cha 48(b) ambayo ni sifa ya lazima
chini ya kifungu cha 39(6) ya kuwa Kiongozi wa Shughuli za
Serikali ndani ya Baraza. Hivyo haitowezekana kuwapata
Wajumbe 2 wa Tume kutokana na kutokuwepo msingi halali wa
kikatiba wa kuwapata;
iii.

Muda wa kujenga uwezo wa kiutendaji na wa kitaasisi:Hata


kama changamoto zilizotajwa hapo juu zitapatiwa ufumbuzi,
changamoto kubwa ni ile ya muda utaohitajika kujenga uwezo
wa kiutendaji kwa Sekretarieti na wasaidizi wao katika ngazi ya
Mikoa na Wilaya na Wajumbe wa Tume ili waweze kusimamia
uchaguzi kwa ufanisi wa viwango vinavyokubalika.
Changamoto nyengine ni ya muda utaohitajika wa Tume
kuhakiki na kujiridhisha na daftari la wapiga kura ambayo ndio
nyenzo kuu ya uchaguzi. Kwa vyovyote vile muda utaohitajika
kwa Tume mpya kujiandaa hadi kufanya uchaguzi mwengine
kwa kiwango cha chini kabisa ni angalau mwaka mmoja. Suala
muhimu ni kwamba nchi itawezaje kwenda wakati hakuna
Baraza la Wawakilishi wala hakuna Baraza la Mapinduzi.
Kutokuwepo kwa Baraza la Mapinduzi kwa maana ya mawaziri
kutaathiri sana utendaji kwa vile mawaziri wana mamlaka
makubwa ya kisheria chini ya Sheria mbali mbali kama vile za
fedha hivyo kutokuwepo kwao au uwepo wao usiokuwa halali
kisheria kuna athari kubwa katika utendaji wa Serikali.
Changamoto kubwa zaidi ni suala la bajeti ya Serikali ambayo
ni lazima iandaliwe na ipitishwe ndani ya muda maalum.

Kwa kuzingatia sababu zote hizo, ni wazi kuwa Hoja ya kurudiwa uchaguzi
haina uhalali, haina msingi na ni chachu ya kuiweka nchi katika utawala
usiokuwa halali na kusababisha fadhaa kubwa kwa wananchi. Ni hoja
ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu katika nchi na kupelekea mzozo
mkubwa zaidi wa kikatiba na kisheria. Sidhani kama tunataka tuifikishe
huko nchi na tuwafikishe huko wananchi tulioapa kuwatumikia na
kuwalinda.

22

5. MAZUNGUMZO YANAYOWAHUSISHA WAGOMBEA URAIS


WA CUF NA CCM PAMOJA NA MARAIS WASTAAFU WA
ZANZIBAR
Kufuatia jitihada kubwa nilizozifanya kwa njia ya simu na hatimaye
kufikisha maombi yangu kwa maandishi kumtaka Dk. Ali Mohamed Shein
akutane na mimi, hatimaye alikubali na kupendekeza tuwashirikishe
viongozi wengine wastaafu wa Zanzibar.
Hadi sasa tumeshafanya vikao vinane, cha kwanza kikiwa ni kile cha tarehe
9 Novemba, 2015.
Wengi wenu mmehoji kwa nini nikakubali kushiriki vikao ambavyo niko
peke yangu kutoka CUF wakati CCM wako watano. Nilikubali hivyo kwa
kutumia msingi wa kuwashirikisha Marais wastaafu wa Zanzibar lakini pia
nikiamini kwamba tungeongozwa na busara na kuheshimu Katiba na Sheria
badala ya utashi wa vyama vyetu.
Tokea mazungumzo hayo yaanze, wananchi wengi wamekuwa wakitaka
tuwaeleze kinachoendelea. Mimi binfasi niliamua kubaki kimya kwa
kuheshimu msingi tuliojiwekea kwamba taarifa ya mazungumzo hayo
itolewe kwa pamoja baada ya mazungumzo kukamilika. Hata hivyo,
inasikitisha kuona wakati mimi nikiheshimu hilo na kuwa kimya kipindi
chote hicho, viongozi wenzangu kutoka upande mwengine wamekuwa
wakiliuka hilo na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikiwachanganya
wananchi.
Kutokana na mwenendo huo, nimeona kuna haja na mimi kuwaeleza
wananchi ukweli wa kile kinachoendelea.
Rais John Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ya kututia moyo ili
tukamilishe mazungumzo hayo kwa ufanisi na kwa kuzingatia matakwa ya
Katiba na Sheria. Alikutana na mimi na baadaye akakutana na Dk. Ali
Mohamed Shein. Hata hivyo, inasikitisha kwamba hata yeye Rais Magufuli
hakuachwa kufitinishwa na wananchi wa Zanzibar pale Balozi Seif Ali Iddi
alipodai hadharani kwamba eti Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katutaka turudi Zanzibar tukakamilishe taratibu za kurudia
uchaguzi, jambo ambalo si kweli.

23

Ukweli ni kwamba katika vikao hivyo vinane bado Dk. Ali Mohamed Shein
na Balozi Seif Ali Iddi wanangangania kurudia uchaguzi huku wakimtetea
kwa nguvu zote Jecha Salum Jecha, na mimi nimesisitiza haja ya kuheshimu
matakwa ya kikatiba na kisheria na maamuzi ya wananchi wa Zanzibar
waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 katika uchaguzi ambao waangalizi
wote wa ndani na nje na hata Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar walisema kwamba ulikuwa huru, wa haki na uliofanyika katika hali
ya amani.
Kwa hakika hadi jana, ukiangalia tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
utaona taarifa zinazosema kwamba uchaguzi hadi hatua ya kuhesabu kura
ulifanyika kwa utulivu nchi nzima.
Kutokana na kutofikia muafaka pamoja, tulikubaliana kuandaa taarifa ya
pamoja ambayo ilielezwa kwamba ingeandaliwa na Katibu wa vikao hivyo
lakini sasa ni zaidi ya wiki mbili, hakuna kikao kilichoitishwa. Nimeandika
barua kuhimiza kikao cha kupokea taarifa hiyo na kuipitisha lakini bado Dk.
Shein anasema wanahitaji muda.
Ni wazi kwamba Dk. Ali Mohamed Shein hakuwa na nia njema katika
mazungumzo haya na amepoteza sifa ya kuongoza vikao hivyo.
6. NJAMA ZA CHINI KWA CHINI ZA KUHUJUMU UTAFUTAJI
WA UFUMBUZI WA HAKI
Wakati Dk. Ali Mohamed Shein akikwepa kwa makusudi kuitisha kikao cha
kupokea taarifa ya mazungumzo hayo, tumegundua kwamba lengo halisi ni
kuisindikiza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutangaza tarehe ya uchaguzi
wa marudio ili baadaye itolewe hoja kwamba suala hilo limeshaamuliwa.
Tunazo taarifa za uhakika kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
imetakiwa kukutana tarehe 14 Januari, 2016 kwa lengo la kutangaza tarehe
ya uchaguzi wa marudio ambao unatajwa kuwa umepangwa ufanyike tarehe
28 Februari, 2016.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba lengo la hatua hiyo ni kukwamisha juhudi
zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa

24

Dk. John Pombe Magufuli, za kutaka kuona ufumbuzi wa haki na


unaozingatia matakwa ya kikatiba na kisheria unapatikana.
Tukiruhusu hatua hiyo maana yake ni kuwaruhusu kikundi cha watu
wachache wanaotumia nafasi zao kujifaidisha kibinafsi na bila ya kujali
maslahi mapana ya nchi na watu wake na wasiojali amani na utulivu wan chi
kututumbukiza katika balaa kubwa sana.
Hivi tunavyozungumza wananchi wa Zanzibar wako taaban na
wamekumbwa na fadhaa baada ya kushuhudia maamuzi yao waliyoyafanya
tarehe 25 Oktoba, 2015 kupitia uchaguzi huru, wa haki na wa wazi yakiwa
yanakanyagwa. Wamesubiri kiasi cha kutosha kwa sababu sisi viongozi wao
tunaojali amani ya nchi tumewataka wasubiri. Sasa umefika wakati
uvumilivu na subira zao zinafikia kikomo. Wanahitaji kuona SUBIRA zao
zinazaa HAKI.
Ni vyema tukaweka wazi wazi hapa kwamba kurudiwa uchaguzi sio
suluhisho na HAKUKUBALIKI. Kwani kama nilivyoonesha, hakuna hoja
wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa.
7. NAMNA BORA YA KUTATUA MZOZO ULIOPO
Kutokana na maelezo ya hapo juu, ni dhahiri kwamba mzozo huu wa
kikatiba na kisiasa ambao umetokana na hujuma zilizofanywa katika
uchaguzi wa Zanzibar haukuwa wa lazima na unaweza kutatuliwa kwa
haraka kama utakuwepo utashi na utayari wa dhati wa kisiasa na wa
kiuongozi ambao unazingatia maslahi mapana na endelevu ya Zanzibar na
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ili kufikia utatuzi huo wa haraka na
unaozingatia na kuheshimu Katiba na sheria ziliopo na misingi ya utawala
bora njia zifuatazo ndizo zitakazotukwamua hapa tulipokwama:
1) Ili kulinda misingi ya Katiba ya Zanzibar inayoelekeza utaratibu wa
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufanya maamuzi kama inavyoelezwa na
kifungu cha 119(1) na (10) na ili kujenga uhalali na heshima ya Tume
katika kutekeleza kazi zake, ni lazima Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar atakiwe kukaa pembeni kwa kujiuzulu au kusimamishwa
kazi hiyo kwa vile amefanya makosa makubwa yafuatayo:

25

a. Yeye kama Mwenyekiti wa Tume hakuwa na mamlaka ya kufanya


uamuzi kwa jambo lolote linalohusu Tume bila ya kupitia vikao
halali vya Tume kinyume na maelekezo ya wazi ya kifungu cha
119(10) cha Katiba ya Zanzibar;
b. Akiwa Mwenyekiti wa Tume ametoa Tangazo Namba 130 katika
Gazeti Rasmi la Serikali linalodaiwa kuwa ni uamuzi wa Tume la
kufuta matokeo ya uchaguzi huku akijua kwamba Tume ya
Uchaguzi haikufanya kikao tarehe 28 Oktoba kupitisha uamuzi
huo;
c. Akiwa Mwenyekiti wa Tume ametoa tangazo la kufuta uchaguzi
huku akijua kwamba hana mamlaka ya kufanya hivyo na akijua pia
kwamba hata Tume ya Uchaguzi haina mamlaka ya kufanya hivyo;
d. Akiwa Mwenyekiti wa Tume amesema uongo hadharani ili
kuhalalisha kitendo chake cha kutoa tamko la kufuta uchaguzi
kama alivyokiri yeye mwenyewe katika kikao cha Tume cha tarehe
1 Novemba, 2015;
Mambo yote haya ni ukiukaji wa Katiba, Sheria na Maadili ya dhamana
aliyokabidhiwa;
2) Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar chini ya Makamu Mwenyekiti na
Makamishna waliobaki wamalizie kutangaza matokeo ya Urais kwa
majimbo 9 ambayo yalishahakikiwa na kumalizia kuhakiki matokeo ya
Urais kwa majimbo 14 yaliyobaki na kutangaza matokeo. Hatimaye
wamtangaze mshindi wa Urais wa Zanzibar. Hatua hii ni halali na sahihi
chini ya kifungu cha 119(10) cha Katiba ya Zanzibar. Aidha, chini ya
kifungu cha 42(6) cha Sheria ya Uchaguzi, hatua hiyo ni halali kwa vile
kifungu hicho kinataka matokeo ya Urais yatangazwe ndani ya siku 3
ama ikiwa kutakuwa na matatizo basi ndani ya siku 3 baada ya matatizo
haya kutatuliwa;
3) Kwa kuwa suala hili ni kubwa na limeathiri taswira ya nchi yetu mbele
ya jumuiya ya kimataifa kwa kiasi kikubwa, na hasa kwa vile Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe
Magufuli, wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya
kukutana na mimi Ikulu Dar es Salaam alisisitiza haja ya kukamilisha

26

mazungumzo na kulipatia ufumbuzi wa haraka, tunaona wakati umefika


yeye mwenyewe aongoze juhudi zenye lengo la kufanikisha hatua
zilizopendekezwa hapo juu;
4) Uongozi wa juu wa Vyama vya CUF na CCM ufanye mazungumzo ya
haraka ya kukamilisha taratibu za kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Zanzibar chini ya mshindi wa uchaguzi wa Urais wa Zanzibar aliyepewa
ridhaa na Wazanzibari kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba,
2015. Kupitia vikao hivyo, kama kuna mambo yoyote yanayohitaji
kujadiliwa na kupata muafaka juu ya uundwaji wa Serikali hiyo
yajadiliwe na kupata muafaka;
5) Mambo yoyote yanayohitaji kurekebishwa katika mfumo wa uchaguzi
wa Zanzibar ili kuondoa kasoro ziliopo kwa nia ya kuimarisha mfumo
huo kwa ajili ya chaguzi zozote za baadaye ni vyema yakawekewa muda
maalum wa kujadiliwa na kupata muafaka.

HITIMISHO
Zanzibar imepita katika siasa za dhoruba na machafuko kwa zaidi ya miaka 50.
Dhoruba na machafuko hayo yalifikia hadi kugharimu maisha ya watu. Ni kwa
sababu ya kuchoshwa na siasa za aina hiyo na migogoro isiyokwisha ndiyo
maana mwaka 2009, mimi na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Karume,
tulichukua maamuzi ya kijasiri ya kuleta MARIDHIANO ambayo yaliituliza
Zanzibar. Kila mmoja wetu ni shahidi kwamba kwa miaka sita iliyopita Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ilipumua kujibu hoja zisizokwisha kuhusu hali ya
kisiasa Zanzibar na badala yake tukawa tunapongezwa kwa kuleta maridhiano
na kuanzisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hatukutegemea
kwamba baada ya kazi ile kubwa, sasa kutazuka kikundi cha viongozi
waliopewa dhamana ya kuwaunganisha watu wafanye kazi ya kuyabomoa
Maridhiano yetu na kuturudisha kwa nguvu kule tulikotoka. Watu hawa
hawapaswi kupewa nafasi kufanikisha dhamira yao hiyo ovu. Na Wazanzibari
hawatowapa nafasi hiyo. Ni kwa sababu hiyo tumeamua kuzungumza na
Watanzania na kuwajuvya haya ili kuzuia nchi yetu isivurugwe na kurudishwa
tulikotoka.

27

Tunaamini kwamba ufumbuzi wa mgogoro uliopo lazima uzingatie Katiba,


Sheria na misingi ya utawala bora. Mapendekezo yaliyotolewa hapo juu ndio
njia pekee ya kuutatua mzozo huo kwa kuzingatia misingi iliyotajwa. Utatuzi
wowote nje ya hapo utakuwa ni wa nguvu na wa utashi wa kisiasa ambao
hautaleta ufumbuzi endelevu na badala yake unaweza kuwa sababu ya mzozo
mkubwa ambao hautaweza kutatuliwa kwa miaka mingi ijayo. Tumuombe
Mwenyezi Mungu tusifike huko.
Mimi na wenzangu tumefanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi wa Zanzibar
na kuwataka watoe nafasi kwa mazungumzo yanayoendelea huku
kuwahakikishia kwamba suluhisho lolote litakalofikiwa litaheshimu maamuzi
yao ya kidemokrasia waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015. Tumefanya hivyo
kwa kutambua wajibu wetu kama viongozi kuhakikisha kwamba Zanzibar na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inabaki kuwa salama. Ni bahati mbaya sana
kwamba wengine wanauchukulia uungwana na ustaarabu wetu kwamba labda
ni dalili ya udhaifu na wanadhani labda wanaweza kutuburuza. Kwa hilo,
nawaambia wazi kwamba WASAHAU. Nataka niwahakikishie kwamba sisi si
dhaifu ila tunaongozwa na uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu na wananchi
wenzetu. Lakini uzalendo huo huo na mapenzi hayo hayo kwa nchi yetu na
wananchi wenzetu yanatutaka tusimame kuitetea na kuilinda Katiba na Sheria
za nchi yetu, haki za raia na maamuzi yao ya kidemokrasia.
Zanzibar kuna tatizo kubwa ambalo halipaswi kuendelea kupuuzwa. Wakati
umefika kwa mamlaka zinazohusika kutokwepa wajibu wao kwa wananchi wa
Zanzibar.
Mimi na wenzangu, kama viongozi twenye dhamana kwa wananchi wa
Zanzibar ambao walitupa ridhaa yao, tunawahakikishia kwamba tutakuwa
tayari kushirikiana nao kuitetea haki yao na maamuzi yao ya kidemokrasia kwa
nguvu zetu zote.
Nawashukuru kwa uvumilivu wenu na kwa kunisikiliza.
Ahsanteni sana.

Vous aimerez peut-être aussi

  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Document20 pages
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Document4 pages
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Document15 pages
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Document20 pages
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Document15 pages
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Document20 pages
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Document20 pages
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Document20 pages
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Document20 pages
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Document20 pages
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Document4 pages
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Document20 pages
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Document11 pages
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Document20 pages
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Document20 pages
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Document20 pages
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Document20 pages
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Document20 pages
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Document20 pages
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Document20 pages
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Pas encore d'évaluation