Vous êtes sur la page 1sur 15

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
TETEMEKO
Wabunge
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.137
51
Toleo No.

Limesambazwa
kwa Taasisi
naTaasisi
Idarana
zote
MEM
, 2015 16 - 22, 2016
Limesambazwa
kwa
Idara
zote MEM Tarehe - 23-29 JanuariSeptemba

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA


Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

abari Uk.2
h
a
m
o
S
TAARIFA KWA UMMA
TUKIO LA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA
3

Kitovu cha Tetemeko la ardhi Kagera (Mduara)


2

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

Nyumba iliyobomolewa na tetemeko la ardhi Bukoba.

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4


Kitovu cha Tetemeko la ardhi Kagera (Nyota nyekundu)

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya News Bullettin
Jarida laGhorofa
Wizarya
a Tano
ya Nishati
au Fika hii
Ofisina
ya Mawasiliano
(MEM) na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

TUKIO LA TETEMEKO LA
ARDHI MKOANI KAGERA
1 Tukio la tetemeko:
Tarehe 10/09/2016 saa 9 na
dakika 27 mchana kumetokea
tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kitovu cha tetemeko hilo ni
kwenye makutano ya latitudo 10 06
na longitudo 31055 eneo ambalo
ni kilomita 20 kaskazini mashariki
mwa kijiji cha Nsunga na kilomita
42 kaskazini magharibi mwa mji
wa Bukoba (Picha Namba 1 na 2).
Kitovu hicho kilikuwa kilomita 10
chini ya ardhi kwenye eneo hilo.
Nguvu za mtetemo wa ardhi wa
tetemeko hilo ni 5.7 kwa kutumia
skeli ya Richter ukubwa ambao
ni wa juu sana kiasi cha kuleta
madhara makubwa. Kutokana na
ukubwa huu maeneo mengi ya
mkoa wa Kagera ikijumuisha mji
wa Bukoba yamepatwa na madhara
makubwa sana ikijumuisha nyumba
nyingi kupasuka (Picha Namba 3
na 4), watu wengi kujeruhiwa kwa
kuangukiwa na vifusi na kuta za
nyuma ambapo inakisiwa kuwa
watu 13 wamepoteza maisha yao.
2 Sababu za kutokea tetemeko hilo:
Kwa kuwa kitovu cha tetemeko
hilo kiko chini sana ya ardhi (Km 10)
na kwa kutafasiri umbile la mawimbi
ya tetemeko hilo yaliyonakiliwa na
vituo vya kupimia matetemeko ya
ardhi (Picka Namba 5) inaonekana
kuwa tetemeko hilo limetokana na
misuguano ya mapange makubwa
ya ardhi iliyopasuliwa na mipasuko
ya ardhi mithili ya mipasuko
kwenye bonde la ufa. Kwa kuwa
eneo lililokumbwa na tetemeko la
ardhi liko karibu na mkondo wa
magharibi wa bonde la ufa la Afrika
Mashariki inakisiwa kuwa mtetemo
huu umesababishwa na kuteleza na
kusiguana ka mapande ya miamba
juu ya mipasuko ya ardhi ya bonde
hilo la ufa.
5

Baadhi ya nyumba zilizobomolewa na Tetemeko la ardhi Bukoba.


3 Upimaji wa matetemeko ya ardhi.
Mapaka sasa na duniani kote
hakuna vifaa au taratibu za kuweza
kutabiri utokeaji wa matetemeko ya
ardhi. Vifaa vyote na taratibu zote
za kuratibu/kupima matetemeko ya
ardhi vinapima ukubwa na tabia ya
tetemeko baada ya tetemeko kutokea.
4 Tafiti za kina.
Wakala wa Jiolojia Tanzania
umepeleka wataalamu katika eneo
la tukio ili kuendelea kufanya utafiti
wa kina juu ya tetemeko hilo. Taarifa
zaidi juu ya tukio hili zitaendelea
kutolewa kulingana na matokeo
ya tafiti hizo pamoja na tafasiri ya
taarifa na takwimu za matetemeko
ya ardhi zinazonakiliwa na vituo vya
kupimia matetemeko ya ardhi nchini
hususan kituo cha Geita ambacho
ndicho kilicho karibu sana na eneo la
tetemeko hili .

Umbile la mawimbi ya tetemeko la ardhi la tarehe 10 Septemba


mkoani Kagera.

5 Mambo Muhimu ya Kuzingatia


Kuepuka Madhara Yanayoweza
Kusababishwa na Tetemeko la Ardhi
i. Kabla ya tukio:
(a) Elimu ya tahadhari
inapaswa itolewe ili kila mmoja
aelewe nini cha kufanya linapotokea
tetemeko la ardhi ikiwa ni pamoja na
kupata mafunzo kutoka kwa watu
wa msalaba mwekundu kuhusu
namna ya kuhudumia majeruhi
ama wahanga na pia jeshi la zima
moto ili kupata elimu kuhusu namna
ya kutumia kizimamoto. Elimu na
mafunzo hayo yatasaidia kuwaweka
watu katika hali ya tahadhari na
hii itasaidia kupunguza taharuki
wakati wa tukio kwa vile watakuwa
sasa wanajua namna ya kuchukua
tahadhari.
(b) Kufanya mazoezi ya
kuchukua tahadhari hizo mara
kwa mara ili kujizoesha kwani
mara nyingi wakati wa matukio
ya majanga kama hayo watu
huchelewa kuchukua uamuzi wa
haraka kujinusuru kwani huwa
bado wanajiuliza kwamba wafanye
nini. Hivyo mazoezi ya mara kwa
mara ya jinsi ya kuchukua tahadhari
humfanya mtu kufanya uamuzi wa
haraka pindi tukio linapotokea.
(c) Wananchi pia
wanashauriwa kujenga nyumba bora
na imara kwa kuzingatia viwango
halisi vya ujenzi, kuweka misingi
imara wakati wa ujenzi, kupata
ushauri wa kitaalamu wa aina ya

majengo yanayofaa kujengwa katika


eneo husika kulingana na ardhi ya
mahali hapo, kuepuka ujenzi wa
nyumba katika miinuko mikali yenye
kuambatana na mawe/ miamba
(suspended boulders) na kuepuka
ujenzi wa makazi katika maeneo tete
yenye mipasuko ya miamba (faults)
na uwezekano mkubwa wa kutokea
matetemeko.
ii Wakati wa tukio:
(a) Wakati wa tukio la tetemeko
la ardhi unashauriwa kukaa mahali
salama kama vile sehemu ya wazi
isiyo na majengo marefu, miti mirefu
na miinuko mikali ya ardhi. Watu
wanashauriwa kukaa nje ya nyumba
katika sehemu za uwazi.
(b) Endapo tetemeko
litakukuta ukiwa ndani ya nyumba
unashauriwa ukae chini ya uvungu
wa meza imara, ama kusimama
kwenye makutano ya kuta na pia
ukae mbali na madirisha na makabati
ya vitabu, vyombo au fenicha ili
kuepuka kuangukiwa na vitu hivyo.
(c) Unashauriwa usitembee
umbali mrefu kwa lengo la kutafuta
mahali salama kwa sababu tetemeko
la ardhi hutokea ghafla na huchukua
muda mfupi. Takwimu zinaonesha
kwamba watu wanaotaharuki na
kukimbia ovyo wakati wa tukio la
tetemeko ndio hupata madhara ama
kuumia.
(d) Salimisha macho yako kwa
kuinamisha kichwa chako wakati wa
tukio.
>>Inaendelea Uk. 3

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

TAHARIRI

Poleni Watanzania
kwa Tetemeko la
Ardhi

Mnamo tarehe 10 Septemba, 2016, lilitokea tukio la


Tetemeko la Ardhi katika Mkoa wa Kagera ambapo
kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), nguvu za mtetemo ni 5.7 kwa kutumia kipimo
cha Ritcher, ukubwa ambao umetajwa kuwa ni wa
juu sana.
Aidha, kutokana na tukio hilo, maeneo mengi
ya Mkoa wa Kagera ikijumuisha mji wa Bukoba
yamepatwa na madhara yakiwemo ya vifo, majeruhi,
nyumba kupasuka na nyingine kuanguka.
Kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya utafiti ya
GST, imeelezwa kuwa, chanzo cha tetemeko hilo ni
msigano wa mapande miamba katika uelekeo wa
Kaskazini kusini uliosababisha kuteleza kwa pande la
miamba kuelekea ulalo wa Mashariki.
Vilevile, baada ya tukio hilo kutokea, GST wametoa
taarifa mbalimbali kuhusu tukio hilo na kueleza kuwa,
tayari timu ya Wataalam ipo mkoani humo kwa
shughuli za Kitaalam ambazo zinahusiana na tukio
husika.
Miongoni mwa Wataalam hao ni pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa Justin Ntalikwa ambaye alipata wasaa wa
kutoa elimu ya namna ya kujikinga kwa wahanga wa
tukio hilo.
Miongoni mwa njia ambazo Prof. Ntalikwa
aliziainisha ni pamoja na kukaa maeneo ya wazi
wakati tukio kama hilo linapotokea, kuingia chini
ya uvungu au chini ya meza ambazo zipo imara na
kukaa katika kona za nyumba.
Aidha, pamoja na elimu iliyotolewa, Wakala huo
umeleeza kuwa, utaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya
tukio hilo kulingana na matokeo ya tafiti zinazoendelea
kufanywa na wataalam hao kupitia vituo vya kupima
mitetemo vilivyopo maeneo mbalimbali nchini na
hususan kupitia Kituo cha Geita ambacho kipo jirani
na Mkoa wa Kagera.
Kutokana na tukio hilo, Wizara ya Nishati na
Madini inawapa pole wananchi wote walioathirika
na tukio hilo ambalo Wataalam wanaainisha kuwa ni
miongoni mwa majanga ya asili.
Aidha, Wizara inawasihi wananchi wote kuzingatia
elimu inayoendelea kutolewa kuhusu namna ya
kujikinga pindi matukio kama hayo yanapotokea.

Septemba 16 - 22, 2016

TUKIO LA TETEMEKO LA
ARDHI MKOANI KAGERA
>>Inatoka Uk. 2

(e)
Baki mahali salama hadi hapo mitetemo
itakapo malizika na kisha ujikague
kuona kama hujaumia na ndipo utoe
msaada kwa wengine ambao watakuwa
wameumia.
(f) Ondoka mahali ulipo kwa
uangalifu kuepuka vitu ambavyo
vitakuwa vimedondoka na kuvunjika
kwani vinaweza kukudhuru.
(g) Jiandae kwa mitetemo
itakayofuata baada ya mtetemo mkuu.
Tetemeko kuu huwa mara nyingi
linafuatiwa na mitetemo mingi midogo
midogo.
(h) Kumbuka kuwa matukio
ya matetemeko ya ardhi huweza
kuambatana na moto hivyo jihadhari
na matukio ya moto kwa vile tetemeko
la ardhi linaweza kusababisha kupasuka
kwa mabomba ya gesi au kukatika
kwa nyaya za umeme ama kuharibika
kwa vifaa vinavyotumia umeme na
kusababisha hitilafu ya umeme.
(i) Kama uko nje ya jengo wakati
tetemeko linatokea unashauriwa kubaki
nje, simama mahali pa wazi na uwe
mbali na majengo, miti mikubwa,
nguzo na nyaya za umeme na ujikinge
kichwani kadri inavyowezekana kwani
paa za nyumba, miti, nguzo na nyaya za
umeme vinaweza kudondoka na kuleta
madhara.
(j) Endapo utakuwa unaendesha
chombo cha moto wakati wa tukio la
tetemeko la ardhi unashauriwa usimame
kwa uangalifu sehemu salama na usubiri
hadi mitetemo imalizike ndipo uendelee
na safari yako kwani tetemeko linaweza
kusababisha barabara au madaraja
kukatika.

(k) Endapo utakuwa kwenye


maeneo ya miinuko au milima uwe
mwangalifu ili kuepuka kuporomokewa
na mawe au kuangukiwa na miti,
(l) Baada ya mitetemo kumalizika
endapo itakulazimu kuondoka
mahali ulipo ukiwa katika jengo refu
unashauriwa kutumia ngazi badala ya
lifti au kipandishi.
iii Baada ya tukio:
(a) Wananchi wanashauriwa baada
ya tukio kuzima umeme katika majengo
ili kuepuka kutokea kwa hitilafu ya
umeme kwani mitetemo huenda
ikaendelea tena.
(b) Kukagua majengo kwa
uangalifu ili kuhakikisha kama
hayakupata madhara kama vile nyufa
n.k,na kwamba yanaweza kuendelea
kutumika na kama ikibidi basi
unashauriwa kuwaita wataalamu wa
majengo ili wayafanyie ukaguzi.
(c) Endapo utaangukiwa na vitu
vizito usijaribu kutumia nguvu nyingi ili
kujinasua kwani hujui vitu hivyo vina
uzito kiasi gani, omba msaada kwa kuita
kwa sauti lakini usifanye hivyo mara
nyingi ili usipoteze nguvu nyingi mwilini
maana hujui ni lini utaokolewa,
(d) Toa msaada unaowezekana
kwa watu walioathirika na tetemeko na
utoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika
na uokoaji.
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
S.L.P. 903
Dodoma
Tanzania
Simu: 0262323020
Tovuti: www.gst.go.tz

KWA HABARI PIGA SIMU


kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
PROF. NTALIKWA AWATEMBELEA
WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati


na Madini, Profesa Justin Ntalikwa,
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Kigazi, Kitongoji cha Bilongo mkoani Kagera
walioathirika na tetemeko la ardhi lilitokea
tarehe 10 Septemba, 2016, mkoani humo,
Prof. Ntalikwa alitoa elimu kwa wananchi
hao kuhusu namna ya kujihami pindi janga
kama hilo linapotokea. Aidha, alizitaja
mbinu ambazo zinaweza kutumika kuwa ni
pamoja na kukaa maeneo ya wazi wakati
wa tukio, kuingia chini ya uvungu wa kitanda
au chini ya meza ambazo zipo imara na
kukaa katika kona za nyumba.

Mtaalam wa Miamba kutoka Wakala wa


Jiolojia Tanzania (GST), Sudian Chiragwile,
akisisitiza jambo kwa waathirika wa
tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa
ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Prof. Justin Ntalikwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya


Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kigazi , Kata ya Minziro Wilaya ya Misenyi
mkoani Kagera ambako kwa Mujibu wa
Wataalam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), wameleeza kuwa eneo hilo ndiyo
kitovu cha tetemeko hilo.

Baadhi ya nyumba ambazo


zimeathirika na tetemeko
hilo.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

GST YATOA TAARIFA UTAFITI WA


AWALI CHANZO CHA TETEMEKO

akala wa Jiolojia
Tanzania (GST),
tarehe 13 Septemba,
2016, ulitoa taarifa ya
utafiti wa awali wa
tetemeko la ardhi baada ya kutembelea
eneo la kitovu cha tetemeko hilo katika
Kijiji cha Kigazi, kilichopo Kata ya
Minziro iliyopo Kilometa 88 Kaskazini
Magharibi mwa Bukoba Mjini.
Utafiti wa GST, umeainisha chanzo
cha tetemeko hilo kuwa ni msigano wa
mapande miamba katika uelekeo wa
Kaskazini kusini uliosababisha kuteleza
kwa pande la miamba kuelekea ulalo wa
Mashariki.
Kutokana na umbile la dunia lilivyo
kwa kufuata kipenyo cha dunia, eneo la
juu ni gumu ambako viumbe, udongo,
maji na hewa unapatikana, eneo lililo

chini ya la juu ni rojorojo na eneo la


katikati ni gumu lililoundwa na madini
ya chuma na nikeli, iliongeza taarifa
hiyo.
Mzunguko wa rojorojo hiyo ni
kusukuma mapande ya miamba yaliyo
juu yake na kusababisha mapande
ya miamba ya ardhi kuachana,
kugongana na kukandamizana. Pindi
miamba iliyopo kwenye mwendokasi
inapongongana na kulazimishwa
kusimama kwa nguvu inasababisha
kupoteza nguvu yake kwa njia ya
kutetetemeka kwa haraka sana
inayoambatana na joto au kishindo.
iliongeza taarifa hiyo.
Vilevile, taarifa hiyo iliongeza kuwa,
matokeo ya kusafiri kwa mawimbi ya
mitetemo ya ardhi ni tetemeko ambalo
linaweza kuleta maafa au upotevu

wa mali. Pia, tetemeko linapotokea


huanza kwa pigo ya awali, tetemeko
kuu na baada ya tetemeko. Mitetemo
inayotokea baada ya tetemeko kuu
la ardhi inaashiria na kupungua kwa
mapande yanayosigana. Ukubwa
wa tetemeko la ardhi unategemea
mwendokasi wa mapande yanayosigana,
kugongana au kusuguana. Ukubwa wa
tetemeko hupungua kadri unapotoka
kwenye kitovu cha ardhi.
Kuhusu vituo vya upimaji wa
vituo vya kurekodi mitetemo, taarifa
hiyo imetaja kuwa, vipo 9 ambavyo
vimesimikwa katika maeneo ya Geita,
Babati, Kibaya, Arusha, Kondoa,
Dodoma, Mtwara na Songwe, na
kuongeza kuwa, vituo hivyo vina uwezo
wa kurekodi eneo lilipotokea tetemeko,
ukubwa wa mwendokasi na kina

STEAG yaonesha nia kuendeleza


Wataalam Makaa ya Mawe
Na Devota
Myombe

ampuni ya
kuzalisha umeme
kwa kutumia
makaa ya mawe
kutoka nchini
Ujerumani ya STEAG
imeonesha nia ya kuendeleza
wataalam kutoka Tanzania
kuhusu teknolojia hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi
wa Huduma za Mtambo
kutoka kampuni ya STEAG,
Achim Nietzschmann
wakati alipokutana na Naibu
Katibu Mkuu katika Wizara

ya Nishati na Madini, Dkt.


Mhandisi Juliana Pallangyo
anayeshughulikia masuala
ya Nishati ili kueleza nia
ya kampuni hiyo kuzalisha
Umeme kwa kutumia makaa
ya mawe.
Mkurugenzi huyo alisema
kuwa, Kampuni hiyo ina
uzoefu mkubwa katika sekta
hiyo kwani imekuwa ikifanya
kazi ya uzalishaji umeme kwa
zaidi ya miaka 75 na imebobea
katika teknolojia ya uzalishaji
umeme kwa kutumia makaa ya
mawe.
Akizungumzia kuhusu
kutoa elimu kuhusu teknolojia
hiyo, Nietzschmann alisema
kuwa kampuni yao iko tayari

kutoa mafunzo na ushauri


kuhusu teknolojia ya uzalishaji
wa umeme kwa kutumia
madini hayo. Tupo tayari
kutoa semina kwa wataalam
wenu endapo Wizara itatupa
kibali alisema Nietzschmann.
Naye Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO),
Zena Kongoi, alisema
kuwa kumekuwa na nia ya
kuendeleza mradi wa kuzalisha
umeme kwa kutumia makaa ya
mawe wa Kiwira wenye uwezo
wa Megawati 200 ila bado kuna
changamoto ya uelewa mzuri
juu ya teknolojia hiyo.
Ni vizuri tukazungumzia
na kuona jinsi tunavyoweza

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),


Zena Kongoi (Wa pili kushoto) akifafanua jambo kwenye kikao cha
kujadili Uzalishaji Umeme kwa makaa ya mawe kilichofanyika hivi
karibuni kwenye Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es
Salaam. Kulia kwake ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia
umeme, Mhandisi Innocent Luoga.

kutoka uso wa dunia palipo chanzo cha


tetemeko.
Pia taarifa hiyo iliongeza kuwa,
Wakala huo umeanza kufanya utafiti
wa kina wa Jiofizikia ili kuweza kubaini
uelekeo na ulalo wa miamba iliyoathirika
na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Taarifa zaidi juu ya tukio hili
zitaendelea kutolewa kulingana na
matokeo ya tafiti hizo pamoja na taarifa
na takwimu za mitetemo ya ardhi
zinazonakiliwa na vituo vya kupima
mitetemo ya ardhi nchini hususan kituo
cha Geita ambacho ndicho kilicho karibu
sana na eneo la tetemeko hili, iliongeza
taarifa hiyo.
Tetemeko l ardhi lenye ukubwa wa
5.7 kwa kutumia Richter lilitokea tarehe
10 Septemba, 2016 saa 9 na dakika 27.

kutumia teknolojia hii maana


hatujawahi kuitumia lakini
tumedhamiria kuitumia na
mkakati ni kuwa ifikapo mwaka
2019-2020 mradi huo uwe
umekamilika, alieleza Kongoi.
Naye, Dkt Juliana Pallangyo
alielezea kuwa mradi wa
uzalishaji umeme wa Kiwira
ukikamilika utakuwa ni neema
kubwa kwa Tanzania kwani
kwa muda mrefu nchi imekuwa
ikitamani kuanzisha mradi
huo lakini bado haujafanikiwa.
Tumepokea kwa shukrani
suala hili kwani imekuwa
shauku yetu kwa muda mrefu
kuzalisha umeme kwa kutumia
madini hayo,alisema Dkt
Pallangyo.
Aidha,Dkt Pallangyo
aliwaagiza wataalam wa
STAMICO pamoja na wizara
kuhakikisha wanaandaa timu
itakayohusisha Wahandisi
kutoka Wizara na Taasisi za

Wizara kwa ajili ya kupewa


mafunzo hayo.
Vilevile, aliwaagiza
wataalam hao kuandaa
mwongozo utakaosaidia
kampuni hiyo kujua mahitaji
ya Tanzania kuhusu teknolojia
ya uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia makaa ya mawe.
Hakikisheni mnaandaa
timu ya wataalam ambao
watapewa mafunzo kuhusu
teknolojia hii, na pia mwongozo
utakaoonesha nini tunahitaji
katika mradi unaoandaliwa
ili Kampuni wajue nini cha
kufundisha katika semina hiyo.
aliagiza Dkt Pallangyo.
STEAG ni kampuni ya
Kijerumani yenye mitambo
yake ya kuzalisha umeme
katika nchi tatu ambazo ni
Colombia, Uturuki na Ufilipino
na inazalisha Megawati 10,300
za umeme.

Meneja kutoka Kampuni ya Uzalishaji Umeme (STEAG),Walter


Englert(Kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo baada ya kumaliza
kikao cha kujadili Mradi wa Uzalishaji Umeme kwa Makaa ya Mawe
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

MRADI WA USAFIRISHAJI UMEME LINDI


MTWARA KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME

ukamilika kwa mradi


wa njia ya kusafirisha
umeme wa msongo
wa kilovolti 132 kutoka
mkoani Mtwara hadi
eneo la Mnazi Mmoja mkoani
Lindi pamoja na ujenzi wa Vituo
vya kupooza umeme vya uwezo wa
MVA 20 katika mji mdogo wa Mnazi
Mmoja mkoani Lindi na kingine
chenye uwezo wa MVA 20 mkoani
Mtwara kutasaidia kuboresha hali ya
upatikanaji na usambazaji umeme
katika maeneo mengi ya mikoa hiyo.
Hayo yamesemwa na Kamishna
Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia
Umeme, Mhandisi Innocent Luoga

hivi karibuni alipofanya ziara ya


kukagua mitambo ya kuzalisha
umeme ya Somanga Fungu (MW
5), mkoani Lindi na Liwale (Kilowati
800) mkoani Mtwara pamoja na
miradi ya umeme vijijini katika
Wilaya za Liwale, Ruangwa na
Masasi kwa lengo la kuangalia
maendeleo ya miradi inayotekelezwa
pamoja na hali ya umeme katika
mikoa hiyo.
Mradi wa njia ya kusafirisha
umeme wa msongo wa kilovolti 132
kutoka Mtwara hadi Mnazi Mmoja
katika Mkoa wa Lindi pamoja na
ujenzi wa vituo vya kupooza umeme
vya MVA 20 unatarajiwa kukamilika

kuwa, Serikali inaendelea na jitihada


za kuunganisha Wilaya ya Liwale na
umeme unaozalishwa kwa kutumia
gesi asilia, jambo ambalo litawezesha
wilaya hiyo kupata umeme wa
uhakika na hivyo kuepukana na
gharama za uzalishaji umeme kwa
kutumia mafuta ya dizeli.
Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga
aliambatana na Wataalam wa Shirika
la Umeme Tanzania ( TANESCO),
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Ahmed
Chinemba na Mkandarasi Kampuni
ya MBH Contractors inayotekeleza
miradi ya umeme vijijini, Wilaya za
Liwale na Ruangwa.

mwezi Februari mwaka 2017.


Aidha akiwa mkoani Mtwara
Kamishna Msaidizi, alitembelea
mitambo ya kufua umeme kwa
kutumia gesi asilia inayozalisha
umeme wa kiasi cha megawati 18
ambayo hivi karibuni ilipata hitilafu
na kuleta changamoto ya upatikanaji
wa umeme wa uhakika katika mkoa
huo.
Taarifa ya Kamishna Msaidizi
Luoga inaeleza kuwa, hali ya
uzalishaji umeme katika mitambo
hiyo inatarajiwa kurejea katika hali ya
kawaida baada ya kazi ya ukarabati
mashine iliyoharibika kukamilika.
Wilayani Liwale, taarifa inaeleza
2

1.
Kamishna Msaidizi
wa Nishati
anayeshughulikia
Umeme, Mhandisi
Innocent Luoga (wa
pili kushoto) akikagua
mitambo ya kuzalisha
umeme kwa kutumia
mafuta ya dizeli
Wilayani Liwale.
2.
Mtambo wa kuzalisha
umeme kwa kutumia
Dizeli

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Wataalam wakati
akikagua ujenzi wa Kituo kipya cha kusambaza umeme wa kiasi cha MVA 20 mkoani Mtwara.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

UKAGUZI WA MIRADI YA
UMEME LINDI NA MTWARA

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi


Innocent Luoga (katikati) akijadiliana jambo na Wataalam alipotembelea
Kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Mtwara.

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme,


Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) akiangalia Mitambo
mbalimbali inayotumika kuzalisha umeme mkoani Mtwara.

Baadhi ya mitambo inayotumika kuzalisha umeme ya Somanga Fungu


mkoani Lindi.

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme,


Mhandisi Innocent Luoga akikagua moja ya eneo
itakapojengwa miundombinu ya usafirishaji umeme wa msongo
wa kV 132 kutoka Mtwara hadi Lindi.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

Kampuni ya Poly Technologies Inc


yatoa msaada wa Taa 2300 za Jua
Na Rhoda James

anzania ni miongoni
mwa nchi 30 za Afrika
ambayo imepokea
msaada wa jumla ya Taa
2300 za Solar kutoka
Serikali ya China kupitia Kampuni
ya Poly Technologies Inc, kwa ajili
ya familia ambazo hazijafikiwa na
umeme wa Gridi ya Taifa.
Hayo yamebainika wakati wa
kikao cha kusaini mkataba wa
msaada huo, ambao ulisainiwa na

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya


Nishati na Madini, anayeshughulikia
Madini, Profesa James Mdoe na Rais
wa Kampuni ya Poly Technologies
Inc, Wang Xingye mwazoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Rais Xingye alisema kuwa,
Serikali ya China inaendelea
kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kwa namna mbalimbali lengo likiwa
ni kuhakikisha kuwa wananchi
wanafikiwa na huduma ya umeme
kwa wakati na popote nchini.
Pia Xingye alisema kuwa

Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia


(Madini), Profesa James Mdoe, (wa pili kulia) akisaini Mkataba
kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wa kupokea msaada wa Taa
2300 za Jua katika kikao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na
Madini, anayeshughulikia (Nishati), Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria upande wa Nishati Anna
Ngowi (aliyesimama), Rais wa Kampuni ya Poly Technologies Inc,
Wang Xingye (wa nne), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Poly
Technologies Inc,Yang Guang (wa tano).

Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia


(Madini), Profesa James Mdoe (wa pili kulia) akipokea Taa ya
Solar kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Poly Technologies Inc,Wang
Xingye (kushoto) mara baada ya kusaini Mkataba huo.

kampuni ya Poly Technologies Inc, ni


miongoni mwa Kampuni 20 kubwa
nchini China na kwa sasa ina mpango
ujulikanao kama Enlighten Africa
ambao unatoa msaada wa Taa za
Solar kwa nchi 30, huku Tanzania
ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe kwa niaba
ya Serikali ameishukuru nchi ya
China kupitia kampuni hiyo ya
Poly Technologies kwa kuendelea

kushirikiana na Serikali ya Tanzania


katika maeneo mengi hususan katika
umeme.
Profesa Mdoe aliihakikishia
kampuni hiyo kuwa, msaada huo
utawafikia walengwa kwa wakati na
kuongeza kuwa maeneo ambayo
yatapata msaada huo yataainishwa
mara baada ya kupokea Taa hizo za
Solar tarehe 30 Septemba, 2016.
Profesa Mdoe alisema kuwa
Serikali ya Tanzania itajifunza mengi
kutoka nchi ya China hasa katika
masuala ya Nishati mbadala.

Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia


(Madini), Profesa James Mdoe (wa pili kulia) na Rais wa Kampuni
ya Poly Technologies Inc,Wang Xingye (kushoto) wakipeana mkono
mara baada ya kusaini mkataba huo. Wengine katika picha ni
Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia
(Nishati), Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Sheria upande wa Nishati Anna Ngowi.

Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia


Madini, Profesa James Mdoe (wa tatu kulia) katika picha ya
pamoja mara baada ya kikao hicho.Wengine katika picha ni Naibu
Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kulia), Rais wa Kampuni ya Poly
Technologies Inc,Wang Xingye (wa nne), Viongozi Waandamizi wa
Wizara ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe wa kampuni ya
Poly Technologies Inc.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU


MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DKT. JULIANA
PALLANGYO JIJINI DAR ES SALAAM KUZUNGUMZIA
MASUALA MBALIMBALI YA SEKTA YA NISHATI

Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa


Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli,Wizara ya
Nishati na Madini mwaka 1985, mara alipomtembelea Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni
ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya,
Jacqueline Kawishe.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia


Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya Idara
ya Nishati katika kikao hicho.
Kutoka kulia, Profesa
Mark Mwandosya, Kaimu
Kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli kutoka
Wizara ya Nishati na Madini,
James Andilile na mwakilishi
kutoka Kampuni ya Pan
African Energy, Jacqueline
Kawishe wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yanatolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo
(hayupo pichani).

Profesa Mark Mwandosya akisisitiza jambo katika kikao hicho

Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli


kutoka Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi
kutoka kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa
katika picha ya pamoja.

10

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

BUSINESS PERSPECTIVE

Email: salum.mnuna@gmail.com

By Salum Mnuna

Salum Mnuna is certified PPP specialist based in Dar es Salaam.


Can be reached via Email: salum.mnuna@gmail.com
The views in the article are solely based on the knowledge of the author and should
not be associated with his employer.

Project Financing Credit risks and its influence on closing


infrastructures investment deals during Negotiations

oing into negotiations


without a prior knowledge
on the subject matter can
be a catastrophic. Going
into negotiation with
preset position of the subject matter
is equally a disaster, position based
negotiations looks at a need to create a
winner, which means leaving one side
as a looser, and I never met anyone
with desire ever to be on a losing side.
Negotiations particularly Business and
investment focused negotiation deals are
backed by numbers and characterized
by appraising the investment initially
looking into information that includes
credit ratings of the project sponsors,
economic, technical, political and
technological dynamics and bankability
of the conceptualized project.
Negotiators from all parts involved
need to present their interest and need
to be focusing on addressing solution to
a certain problem the investment will
address. Solution focused negotiations
brings all parts interests into common
understanding which will create an
environment that will leave no loser
when finalizing the investment deal.
Understanding that basic information
surrounding the nature of the deal,
sponsors, investors and interests
of financiers on that particular
infrastructure nature prior negotiation
can mitigate some risks of breaking
down negotiation engagements.
When speaking of infrastructure
investment deals, you cannot ignore
the role of the multilateral banks,
Credit agencies and other local and
international commercial banks as
primary lenders to the project financed
infrastructure investment. What
information primarily demanded by
these agencies from project sponsors
and association borrowers to the
project company? Being an Ex-bank
staff myself, I have witnessed it on the
first hand at the Commercial bank
Standards. Banks do not have money
of their own, banks keeps customer
deposit and lends it at interest rate
higher than what they give to depositors.
Banks do not and will not lend to
customer or project that is perceived

too risky to meet its future obligations


or not bankable. Decision makers and
interested borrowers need to understand
lenders decision boundaries in order to
reach out conclusions that are effective
and that works for benefits of all. The
negotiators needs to seek trusted and
reliable information, these could help
minimize heat inside discussion room
and lights a path to mutual benefiting
consensus. Emotions or lack of
information, guesswork and accusations
certainly not amongst requirements
needed in working out to getting close to
the business infrastructure deals.

construction risk, operational risk,


offtake risk and political risk. Financiers
will always demand Project participants
to be clear on the method as mitigates
to manage these risks including political
risk insurance, offshore reserve accounts
and turnkey construction contracts. This
information amongst other underlines
the basis for discussions and decisions
making prior getting into Project
financing led infrastructure business
deals.

Building Win-Win and closing


deals benefiting to all parts
Understanding project financing
Project Financing and Credit risk
structure, Players interests and risks
Project financing a term used
involved in the entire project financing
to describe financing arrangements
cycle can easy processes of each part
between different funding sources and
to define their interests and eventually
project owners. It is in my interest to
become with positions that work and
narrow the discussions on how is this
suits to all parts. Short of understanding
knowledge being perceived and applied
project financing and credit, risks could
in an environment familiar in my
delay or halt any mega infrastructure
territory. Project finance, debt payment
project development plans. No financier
will be solely depended on Project
or investors will ever put funds on project
company projection on generated
financing with clear certainty that the
cash flow as security to a loan unlike
project company would not be able to
traditional corporate financing which is
generate enough cash flows to meet their
based on the history of cash flow and
debt obligations to lenders. Public sector
balance sheet size. The project financing players need to define their interests on
structured deals also put technical,
participations, know their problem and
technological and economical dynamics understand solution when negotiating
considerations in perspective in assessing and continue defending them during
potential opportunities and risks in
operations to ensure value for money
specific infrastructure deals. On the
of the public investment. Incompetency
other hand project financing credit risk
and emotions are functions of poor
is the risk of default on a debt that may
preparations and certainly do raise
arise from a project company failing to
temperature inside negations room and
make required payments obligations.
can lead to people focused discussions
Export Credit Agencies, Multilaterals,
rather than common solution centered
International banks, Domestic banks
discussions.
and Capital markets will always need
The world of investments works on
some sort of assurance on Project
the standards, the participants ought
company ability to generate cash flows
to learn on those existing standards,
and risks mitigation measures taken
accept or reject. Being in between of the
by parts. Structuring infrastructure
accepting and rejecting does not send
financing could be complex exercise
good signals to other participants; not
that demands clear understanding
understanding or knowing is neither a
from all the parts involved, short of
good excuse in the negotiation room
that can increase the risks to the project
nor acceptable reason. Participants
development. An overview of the typical should be on top of their interests and
risks of a project finance transaction
send right individuals to present and
that could affect companys ability to
defend their interests. Right individuals
meet its debt obligations, including
are not assessed on the hierarchy, title

or academic superiority one hold.


Readiness, continues preparations,
passions, ownership, good relationships
and having good knowledge on
technical and economics dynamics
of the specific project deal can define
ones competency, minimize costs and
serve project schedule whilst building
consensus that meet or exceed every
participating part expectations. The
weaker the other side the advantage to
other participants, very rare situation
where you can find one-deal participants
take into considerations other players
interest as their own interest unless
otherwise contributes on their interest
to some degree. If need some time
when capacity is not available internally
from one player, consultancy like
transactional, legal or commercial
advisers should be hired to present
and defends the interest as specified
by the hiring parts. Personal qualities
like Integrity and ownership from the
participating individuals would certainly
contribute to the effectiveness into
getting and closing beneficial deals for
all participating parts. Participating parts
needs to quantify value, understand
what their win means, and present
in win-win situation. Each Win in a
win-win situation has value and it is the
responsibility of every part to attach a
value on their win. Not knowing your
value and yet demanding win-win can
serious damage participating reputations
and sometime hinder negotiations
progress. Negotiations brings in different
departments and wide spectrum
knowledge and skills in one room with
desire to fill in gaps. Individual group
with same interest need to understand
their interests, functions, roles and limits
and the information surrounding the
deal before and during negotiations.
Infrastructure deals presents both
national interests and investors interests
participating parts ought to understand
these and defend both. Bearing in
mind private investors interests are
widely considered national interests to
any country with desire to grow her
economy for development.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

11

12

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Septemba 16 - 22, 2016

TMAA expands laboratory services through SMMRP


n ISO/IEC 17025 Accredited Laboratory
By Greyson Mwase,
Dar es Salaam

he Tanzania Minerals
Audit Agency (TMAA)
is a semi-autonomous
institution established in
2009 under the Executive
Agencies Act, Cap. 245. The aim of
TMAA is to maximize Government
revenue from the mining industry
through effective monitoring and
auditing of mining operations and
ensuring sound environmental
management. TMAA is the successor
of the Minerals Auditing Section
under the Ministry of Energy and
Minerals which was responsible for
undertaking gold auditing of the
major gold mines in the Country.
The Ministry of Energy and
Minerals through the Sustainable
Management of Mineral Resources
Project (SMMRP) has been
supporting the TMAA by providing
new laboratory equipment.
Describing the TMAA Laboratory,
the Manager for Laboratory Services,
Engineer Mvunilwa Mwarabu, says
The Agency has a modern laboratory
which provides laboratory services
on behalf of the Government as well
as commercial services for mineral
explorers, miners, mineral traders,
buyers and exporters.
She adds TMAA Laboratory
receives all sorts of mineral ores,
concentrates, bullions, rock and soil
samples from individuals as well as
corporate entities to ascertain mineral

contents.
The main objectives of the TMAA
include improving delivery of quality
services, improving auditing of
quality and quantity of produced and
exported minerals, and strengthening
the auditing of capital investment and
operating expenditures of large and
medium scale mining entities.
Other objectives are strengthening
the auditing and monitoring of
environmental management of large,
medium and small scale mines,
strengthening management of
information on minerals produced
and exported by large, medium and
small scale mines and strengthening
the mechanisms for minerals royalty
collection from large, medium and
small scale mines.
Explaining the roles and functions
of TMAA, Mwarabu says that the
agency monitors and audits the quality
and quantity of minerals produced
and exported by large, medium and
small scale miners to determine
revenue generated and thus facilitate
collection of payable royalties. It
audits capital investment and
operating expenditure of the large and
medium scale mines for the purpose
of gathering taxable information and
provide the same to the Tanzania
Revenue Authority (TRA) and other
relevant authorities.
We also monitor and audit
environmental management,
environmental budget and expenditure
for progressive rehabilitation and
mine closure, Mwarabu says. She
adds that the agency also collects,
analyzes, interprets and disseminates

Manager for Laboratory Services at Tanzania Minerals Audit Agency


(TMAA), Engineer Mvunilwa Mwarabu explains the contribution
of the Sustainable Management of Mineral Resources Project
(SMMRP) to the expansion of laboratory services at the Agency.

Manager for Laboratory Services at Tanzania Minerals Audit


Agency (TMAA), Engineer Mvunilwa Mwarabu shows the electronic
balance machine donated by the Sustainable Management of
Mineral Resources Project (SMMRP)
minerals production and export data
for projecting government revenue,
planning purposes and decision
making in the administration of the
mining industry.
Mwarabu further explains that the
TMAA advises the government on
matters relating to the administration
of the mineral sector, with a main
focus on monitoring and auditing
of mining operations to maximize
government revenues as well as
conducting research in the mineral
sector that will lead to increased
government revenues.

Major mines audited by the


TMAA include Bulyanhulu (gold),
Buzwagi (gold) Geita (gold),
Golden Pride (gold) North Mara
(gold), Tulawaka (gold) Tanzanite
One (tanzanite) and Williamson
Diamonds (diamonds)
Mwarabu emphasises that the
TMAA provides laboratory services
through its modern laboratory which
provides commercial services to
mineral explorers, miners, mineral
traders, buyers and exporters.
The laboratory receives different
sorts of mineral ores, concentrates,

Engineer Oscar Kalowa from the Tanzania Minerals Audit


Agency (TMAA), explains the use of an XRF machine for mineral
identification that has been donated by Sustainable Management
of Mineral Resources Project (SMMRP)

13
TMAA expands laboratory services through SMMRP

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Manager for Laboratory Services at Tanzania Minerals Audit Agency


(TMAA), Engineer Mvunilwa Mwarabu explains the use of a
SMMRP-donated cupellation furnace for assessing impurities in a
gold bullion sample.
>>From pg 12
bullions, and rock and soil samples
from individuals as well as corporate
entities to ascertain their mineral
content.
The Laboratory also provides
identification and grading of
diamonds and coloured gemstones,
Mwarabu says.
She further explains that most
people prefer using the TMAA
laboratory because it is operated
with qualified, skilled, experienced
and committed staff as well as
modern equipments utilizing the
best technology. Quick and accurate
analysis results in high customer
satisfaction.
Highlighting the services offered
by TMAA laboratory, Mwarabu
says they include sampling, sample
preparation, moisture determination,
drying, determination of gold and
silver content in bullion, and analysis
of soil, concentrate and geological/
exploration samples using fire assay
with gravimetric or AAS finish.
Other services include the gold
quick acid test, rock and mineral
identification, jewellery verification for
gold (karat value) and identification
and grading of diamonds and
coloured gemstones.
Other services may be offered as
per customer requirement, she adds.
Upgrading of the TMAA
laboratory has been achieved with
new equipments provided by the
Sustainable Management of Mineral
Resources Project (SMMRP). These
equipments have enabled the agency
to provide services meeting the
highest technology standards which

contributed to the accreditation of the


International Standard Organization
Certificate (ISO/EIC 17025).
She adds that the agency has
been using appropriate validated test
methods that incorporate adequate
quality control as well as maintaining
all laboratory data and records
generated in appropriate manner that
is easily accessible.
We thank the SMMRP for
the laboratory equipments because
previously we were not working in a
very good condition due to the poor
machines, but now we have new
laboratory equipment with the newest
technology that helps us provide
service in a timely and accurate
manner, Mwarabu emphasises.
Mwarabu further notes that the
laboratory can serve many people at
once, adding that, due to the demand
of services, the laboratory is currently
serving large and medium scale
mining companies as well as small
scale mining companies and mineral
traders.
We have modern an XRF
machine and a pulveriser that can take
more than three samples at once based
on the quantity of the sample, she
adds.
Future needs include more
accessories for the machines they are
using for laboratory services as well
as funding for additional equipment
based on their specifications
requirements.
She thus asking the World Bank
(WB) though the SMMRP to provide
a modern building with enough
space because the building they are
using cant accommodate all staff and
equipment.

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

Manager for Laboratory Services at Tanzania Minerals Audit Agency


(TMAA), Engineer Mvunilwa Mwarabu explains the use of a Niton
FXL FM-XRF Analyzer that has been contributed by the Sustainable
Management of Mineral Resources Project (SMMRP)

Engineer Abdul Milandu from the Tanzania Minerals Audit Agency


(TMAA) explains the use of a hot plate for parting of gold and
silver that has been donated by the Sustainable Management of
Mineral Resources Project (SMMRP)

Head of Communications Unit in Tanzania Minerals Audit


Agency (TMAA), Engineer Yisambi Shiwa, explains the use of the
mobile gemstone lab that has been donated by the Sustainable
Management of Mineral Resources Project (SMMRP)

14

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Denmark, Ujerumani Zajadili


ujenzi Kiwanda cha Mbolea- Kilwa

Sehemu ya Mabalozi na Wawakilishi kutoka katika nchi za Denmark


na Ujerumani wakifuatilia kwa makini maelekezo yaliyokuwa
yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe ( hayupo pichani)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini


anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) na Kaimu
Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini, James Andilile
(kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Balozi wa
Denmark Nchini, Einar Jensen (hayupo pichani)

Na Greyson Mwase

Tanzania, (TPDC).
Akizungumza katika kikao hicho
kilichokutanisha
pia watendaji kutoka
aibu Katibu Mkuu wa
Mamlaka
ya
Udhibiti
wa Huduma za
Wizara ya Nishati na
Nishati
na
Maji
(EWURA)
na TPDC,
Madini anayeshughulikia
Balozi
wa
Denmark
Nchini,
Einar
Madini, Prof. James
Jensen
alisema
kuwa
mara
baada
ya
Mdoe amekutana na
kukamilika
kwa
kiwanda
cha
mbolea,
Mabalozi kutoka nchi za Ujerumani
Tanzania itapata manufaa makubwa
na Denmark ikiwa ni mwendelezo
ikiwa ni pamoja na ajira, fedha za
wa maandalizi kwa ajili ya ujenzi
kigeni kutokana na kuuza mbolea nje
wa kiwanda cha mbolea wilayani
ya nchi na hivyo kuinua uchumi wa
Kilwa mkoani Lindi. Mbolea hiyo
nchi.
itatengenezwa kutokana na gesi asilia.
Wakati huohuo Naibu Katibu
Kiwanda hicho kitamilikiwa na
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
kampuni za Ferrostaal Industrial
Madini anayeshughulikia Madini, Prof.
Projects ya Ujerumani, Haldor Topsoe James Mdoe alisema kuwa maandalizi
ya Denmark na Fauji Fertilizer
kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho
Limited ya Pakistan kwa kushirikiana bado yanaendelea ikiwa ni pamoja na
ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.
na Shirika la Maendeleo ya Petroli

Kutoka kulia Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen, Naibu Katibu


Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Juliana Pallangyo, Mwakilishi kutoka kampuni ya Ferrostaal
Industrial Projects,Wilfried Wiemann na mwakilishi kutoka Ubalozi
wa Denmark, Mette Melson wakiwa katika picha ya pamoja.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini


anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe (aliyekaa mbele)
akiongoza kikao kilichoshirikisha Mabalozi kutoka katika nchi za
Ujerumani na Denmark pamoja na watendaji kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam

Balozi wa Denmark Nchini, Einar


Jensen akieleza jambo katika
kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa


Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini, Prof.
James Mdoe akielezea fursa
za uwekezaji kwenye Sekta ya
Madini nchini.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 16 - 22, 2016

15

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI YASITISHA KWA MUDA


UTOAJI RUZUKU AWAMU YA TATU
Tarehe 20 Julai, 2016, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa Tangazo kwa Umma
kuhusu Kukaribisha Maombi ya Ruzuku Awamu ya Tatu kwa Wachimbaji Wadogo
wa Madini nchini.
Fomu za maombi ya ruzuku hiyo zilitolewa katika Ofisi za Madini za Kanda (ZMO)
na Mikoa (RMO) zikiambatana na vipeperushi maalum vinavyoeleza mambo yote
yanayohusu ruzuku. Fomu hizo zilianza kutolewa tarehe 20 Julai, 2016 na ukomo
wake ulikuwa tarehe 9 Agosti, 2016, saa 9:30 Alasiri.
Wizara inatoa taarifa kuwa, imesitisha kwa muda utoaji wa Ruzuku Awamu ya Tatu
ambao ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 19 Septemba, 2016, hadi pale Tathmini
ya fedha ya Ruzuku Awamu ya Kwanza na ya Pili itakapofanyika.
Aidha, tathmini hiyo itafanyika sambamba na uhakiki wa shughuli za Wachimbaji
Wadogo walioomba Awamu ya Tatu, lengo likiwa ni kujiridhisha kama Ruzuku hizo
zimetumiwa na walengwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Imetolewa na;
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Tarehe 16 Septemba, 2016

Vous aimerez peut-être aussi