Vous êtes sur la page 1sur 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Simu: +255-22-2112035/40 9 Barabaraya Ohio


Nukushi: +255- S.L.P. 9223
2122617/2120486 11483 DAR ES
Baruapepe: ps@moha.go.tz SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Zimekuwepo taarifa za kuingia nchini kwa wahamiaji haramu
kupitia mpaka wetu na Nchi ya Kenya. Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji inawahakikishia
Watanzania kwamba hatua kali za kisheria zinachukuliwa
dhidi ya raia wote wa kigeni wanaoingia nchini kinyume cha
Sheria za Uhamiaji na nchi yetu.

Kimsingi hakuna raia yeyote wa kigeni anayeruhusiwa kuingia


nchini kwa kisingizio cha kuja kufanya kazi, biashara au
Uwekezaji bila kufuata Sheria na taratibu za Uhamiaji, na
kwamba wote wanaokiuka Sheria hizo watarudishwa makwao
mara moja.
Ni jambo lisilokubalika mtu atoke nchini kwake bila kibali cha
kufanya kazi Tanzania kwa madai kwamba alishatuma maombi
ya kibali husika na amekuja kusubiri majibu ya kibali hicho
akiwa Tanzania. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
haitavumilia ukiukwaji huu wa sheria za nchi na kwamba kila
raia wa kigeni anayekusudia kuingia nchini ahakikishe ana
kibali cha kuingia nchini na anafanya kazi ambayo ndiyo
aliyoiombea kwenye kibali chake.

Yapo matukio ya raia wa nchi jirani, hususan katika mipaka ya


Kenya na Uganda ambapo kutokana na hali ya muingiliano wa
kiuchumi na kijamii, raia wa nchi zetu, wamekuwa wakivuka
mipaka pande zote kufuata huduma mbalimbali, Hii pia
inachangiwa na mapungufu katika usimamizi wa alama na
maeneo ya wazi ya mipaka yetu. Hali hii inapelekea baadhi ya
wananchi wetu kutumia mwanya huo kuwatengenezea raia wa
kigeni mazingira ya kuingia nchini bila kufuata taratibu au hata
kutumiwa katika biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Tahadhari inatolewa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa
wakiwapokea raia hao wa kigeni na kuwahifadhi, kwani
kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi ikiwemo ile Sheria ya
usafirishaji haramu wa binadamu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya


Uhamiaji imeanza kuchukua hatua ili kuweza kushughulikia
suala hili. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala,
tayari ametembelea baadhi ya maeneo ya mipaka yetu hususani
kijiji cha Jasini wilayani Mkinga mkoani Tanga ili kujionea hali
halisi na kutoa Maelekezo ya hatua za kuchukua kudhibiti hali
hiyo kwa mujibu wa Sheria, kwa kuwa eneo hilo linaonyesha
kuwa na muingilino baina ya nchi ya Kenya na Tanzania kwa
muda mrefu.

Wizara itaendelea na Mashauriano na Mamlaka nyingine zenye


dhamana ya Kusimamia alama za mipaka ya nchi yetu kwa
kuwa tatizo hili la muingiliano wa wananchi wa pande zote lipo
kwenye mipaka mingi ya nchi.

Imetolewa na
Christina R. Mwangosi
Kaimu Msemaji
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4 Agosti 2017

Vous aimerez peut-être aussi