Vous êtes sur la page 1sur 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 0262322761-5 Ofisiya Bunge


Fax No. +2550262324218 S.L.P 941
Email:info@bunge.go.tz DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


________
Mhe. Spika Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Maalim Seif Sharif
Hamad yenye maelezo ya kuwafuta uanachama wabunge wawili, Mhe.
Magdalena Hamisi Sakaya na Mhe. Maftaha Abdallah Nachuma. Aidha,
Maalim Seif Sharif Hamad amedai kwamba kwa hatua hiyo wamekosa sifa
za kuendelea na ubunge.

Hata hivyo Ofisi ya Spika inayo barua ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
CUF, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba yenye Kumbukumbu Namba
CUF/AK/DSM/MKT/05/2017 ya tarehe 22 Machi, 2017 ikiliarifu Bunge kuwa
Maalim Seif Sharif Hamad ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama
Katibu Mkuu hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu
yatatekelezwa kuanzia tarehe hiyo na Mhe. Magdalena Sakaya (Mb).

Barua hiyo pia ilikuwa na kiambatanisho cha ridhaa ya mabadiliko hayo kwa
barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Ofisi ya Spika haijawahi kupokea barua
yoyote ikielezea vinginevyo. Aidha, Ofisi ya Spika imenakiliwa katika barua ya
Msajili wa Vyama vya Siasa kwenda kwa Maalim Seif Sharif Hamad akisisitiza
kutokuwepo na mabadiliko mengine.
Hivyo basi, Mhe. Spika amemuandikia Maalim Seif Sharif Hamad kwamba
anasita kuifanyia kazi barua yake kutokana na taarifa za awali alizozipokea.

Imetolewa na:
Ofisi ya Spika
S. L. P 941
DODOMA

4 Agosti 2017.

Vous aimerez peut-être aussi