Vous êtes sur la page 1sur 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 026 2322761-5 Ofisi ya Bunge


Fax No. +255 026 2324218 S.L.P. 941
E-mail: info@bunge.go.tz DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


__________

Ofisi ya Bunge ingependa kutolea ufafanuzi kuhusu kauli ya Spika wa Bunge,


Mheshimiwa Job Ndugai aliyoitoa mapema leo Bungeni kuhusiana na suala la
matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu tofauti na
maelezo yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya wanasiasa


zinaeleza kwamba Mheshimiwa Spika ameliongopea Bunge na Watanzania
kuhusiana na gharama za kumsafirisha Mheshimiwa Lissu kwenda Mjini Nairobi
Nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu.

Alichokizungumza Mheshimiwa Spika ni kwamba taratibu zote za ndege


iliyompeleka Mheshimiwa Lissu Nchini Kenya ziliratibiwa na Kamishna wa Tume ya
Utumishi wa Bunge, Mheshimiwa Salim Hassan Turky ambaye ndiye aliyechukua
dhamana ya safari hiyo na taratibu ambazo Bunge ilisaidia. Taratibu hizo ni pamoja
na kupata vibali vyote vya safari ya ndege kuruka nje ya muda uliopangwa katika
Kiwanja cha Ndege Dodoma na kupata haki ya kutua katika Uwanja wa Ndege
Nairobi.

Vilevile ndege hiyo ilikuja kwa mkopo ambao ulidhaminiwa na Mheshimiwa Turky
ambapo deni hilo limelipwa leo baada ya kauli ya Mheshimiwa Spika Bungeni.

Ofisi ya Bunge inawaomba wanasiasa ambao hawafahamu ukweli juu ya jambo


hili waliachie Bunge liendelee kushirikiana na familia ya Mheshimiwa Lissu pamoja
na Uongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ili kuweza kumpatia huduma
anazostahiki wakati huu anapoendelea na matibabu huko Nairobi. Aidha, pale
ambapo taratibu zitaruhusu ili aweze kupelekewa katika Hospitali zinazotambulika
na Serikali kwa matibabu, Bunge halitosita kugharamia matibabu hayo.

Imetolewana:

Ofisi ya Spika,
S.L.P 941.
DODOMA.

14 Septemba,2017.
1

Vous aimerez peut-être aussi