Vous êtes sur la page 1sur 2

WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINI

(RITA)

TAARIFA KWA UMMA

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USAJILI NA KUTOA VYETI VYA


KUZALIWA KWA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KATIKA MKOA WA
LINDI NA MTWARA
(TAREHE: 26 SEPTEMBA - 2 OCTOBA, 2017)

1) UTANGULIZI:

- Zoezi la Usajili linaendelea vizuri


- Zaidi ya nusu ya watoto (57%) wamesajiliwa kwa kipindi cha wiki moja
- Changamoto ya kujua majina yanavyoandikwa yajitokeza

Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 13 ya wananchi wamesajiliwa na


kupata vyeti vya kuzaliwa hivyo Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeendelea kuchukua
hatua katika kukabiliana na changamoto hii .

RITA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imebuni Mpango wa Usajili na Kutoa vyeti vya
Kuzaliwa kwa watoto wa Umri chini ya Miaka Mitano ambao umeanza na unaendelea kutekelezwa
katika Mikoa saba ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Geita na
Shinyanga na hivi karibuni umezinduliwa katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. Kabla ya kuanza
utekelezaji, watoto waliosajiliwa mkoa wa Lindi walikuwa asilimia 11.4 na Mtwara asilimia 9.4.

Mpango huu ulibuniwa ili kuleta suluhisho la changamoto zilizokuwa zikisababisha watoto
kushindwa kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa wakati ambapo msingi wake mkuu
umejengwa katika kusogeza huduma za usajili karibu na makazi ya wananchi hivyo kupatikana
katika Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto.
Vile vile huduma hii hutolewa bila malipo na taarifa za usajili huingizwa katika programu maalum
iliyowekwa kwenye simu za kiganjani (mobile app) na kutumwa kwenye kanzidata ya Wakala.

2) MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Mpango wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wa Mikoa ya Mtwara na Lindi
ulizinduliwa Rasmi tarehe 26 Septemba 2017 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe aliyemwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi na kuanza kutekelezwa katika Halmashauri zote 16 za Mikoa hiyo.
Kabla ya kuanza utekelezaji Wasajili Wasaidizi ambao ni Maofisa Watendaji kata na Wahudumu wa
vituo vya Tiba walipewa mafunzo ya kina ya siku tatu kuhusu Usajili wa vizazi, uhakiki wa
viambatisho, utambuzi wa walengwa, kutuma na kutunza kumbukumbu.

Kufikia leo ni wiki moja tangu kuzinduliwa kwa mpango huu, takwimu zinaonesha watoto 170,493
ya watoto wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ambayo ni asilimia 57 ya watoto 297,269
wanaotakiwa kusajiliwa kwa Mikoa yote miwili.

Ukilinganisha kwa Mikoa, Mtwara inaongoza kwani imeweza kusajili asilimia 60 ambayo ni watoto
106,712 kati ya 179,296 wanaotakiwa kusajiliwa huku Lindi ikisajili watoto asilimia 54 ya watoto
117,972 wanaotakiwa kusajiliwa. Kwa upande wa jinsia, wanawake wamesajiliwa zaidi katika
mikoa yote miwili ( Mtwara 50.3% na Lindi 50.4%) kuliko wanaume japokuwa tofauti kati yao ni
ndogo.

Vilevile Takwimu zinaonesha kwamba Halmashauri 3 bado ziko chini ya wastani wa asilimia 50 ya
waliosajiliwa ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kwa Mkoa
wa Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kwa Mkoa wa Mtwara.

Halmashaui ya Mji wa Newala inaongoza kwa Mkoa wa Mtwara kwa kusajili asilimia 77 ya watoto
na kwa Mkoa wa Lindi, Halmashauri inayoongoza ni ya Ruangwa ambayo imesajili asilimia 73.

3) CHANGAMOTO:

Changamoto kubwa iliyojitokeza ni wazazi na walezi kutokujua kwa usahihi baadhi ya majina ya
watoto wao yanavyoandikwa wakifahamu zaidi kuyatamka japokuwa walielekezwa anayesajili
afike kituoni akijua majina sahihi ya mtoto na wazazi wote wawili. Hali hii imesababisha kupoteza
muda kwani wazazi hupewa muda wa kujiridhisha. RITA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi
kuhusu suala hili.

4) HITIMISHO:

Nusu ya watoto wa umri chini ya Miaka Mitano wameweza kusajiliwa kwa kipindi cha siku saba za
mwanzo na haya ni mafanikio makubwa ikilinganishwa na lengo lililowekwa la kuwasajili watoto
wote kwa kipindi cha miezi mitatu. RITA, Wadau wa Maendeleo na Viongozi katika ngazi ya Mkoa,
Wilaya na Halmashauri tunaendelea kufuatilia na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mpango
huu na ikiwezekana kuwasajili watoto wote ndani ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya
kuzinduliwa kwa mpango huu.

RITA inatoa shukrani kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Wakuu wa Mikoa yote miwili Mtwara na
Lindi, Viongozi wengine wa Mikoa hiyo na wadau wa maendeleo ambao ni Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Serikali ya Canada kupitia Shirika la Idara ya
Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo (DFATD) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya TIGO .
Tunawashukuru, Tunatambua na Kuthamini mchango wao katika kufanikisha utekelezaji wa
mpango huu.

Josephat Kimaro
Meneja Masoko na Mawasiliano

03 Octoba 2017

Vous aimerez peut-être aussi